Mahafali imeandaliwa na idara ya shule za wasichana Alkafeel chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba takatifu, ikiwa na kauli mbiu isemayo (Kutokana na nuru ya Fatuma –a.s- tunaangaza ulimwengu), kwa ushiriki wa wanafunzi elfu 5 kutoka vyuo vikuu tofauti vya Iraq na baadhi ya nchi za kiarabu na kiislamu.
Utoaji wa zawadi hiyo ni sehemu ya kujenga hamasa kwa wahitimu, kwani ni ujumbe wa wazi kwa wote kuwa hakuna kisichowezekana, kila kikwazo kinaweza kuwa hatua ya kuelekea kwenye mafanikio.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya mahafali ya wahitimu (mabinti wa Alkafeel), kwa lengo la kujenga hamasa kwa wahitimu wanaokamilisha safari ya masomo na kuanza maisha ya kufanya kazi wakiwa sehemu hii ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).








