Ibada ya usomaji wa dua imefanywa katika mazingira tulivu na kwa ushiriki wa idadi kubwa ya zuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya wameandaa mazingira vizuri kwa ajili ya ibada hiyo tukufu ambayo hufanywa kila wiki, wameandaa vitabu vya dua, sehemu maalum ya kufanyia idaba, wamepuliza marashi sehemu hiyo sambamba na kutoa huduma zingine nyingi.



