Tambua huduma kuu zinazotolewa na idara ya mashahidi na majeruhi

Idara ya mashahidi na majeruhi chini ya Atabatu Abbasiyya inatoa huduma mbalimbali kwa familia za mashahidi na majeruhi.

Kiongozi wa idara Sayyid Ahmadi Twayari amesema: “Idara inatoa huduma mbalimbali, miongoni mwa huduma hizo ni, kuandaa utaratibu wa kisheria kwa kushirikiana na pande husika, kutoa misaada ya kimali na kibinaadamu, kutembelea familia za mashahidi, kuweka visa vyao kwenye vyombo vya habari na kuonyesha ukubwa wa kujitolea kwao”.

Akaongeza kuwa: “Idara imetoa broshua (kijitabu elezi) inayofafanua kazi zinazofanywa na idara pamoja na namna ya kuwatambua ndugu wa mashahidi na majeruhi, kwa lengo la kuweka uangalizi kamili na kutoa huduma kwao”.

Akasema kuwa “Broshua ni muhimu kwa kuimarisha mawasiliano na familia za mashahidi na kufafanua huduma wanazofaa kupewa kwa uwazi”.

Chapisho hilo linaonyesha jitihada za idara katika sekta ya habari na kuthibitisha uwepo wake na huduma za kibinaadamu zinazotolewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: