Kuadhimisha kumbukizi ya mazazi ya Bi Fatuma Maasuma (a.s) katika mji wa Baabil

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, wamefanya program ya kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Maasuma (a.s) katika mkoa wa Baabil.

Program hiyo imefanywa kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa mazaru wa Imamu Qassim bun Mussa Alkadhim (a.s), na kuhudhuriwa na kundi kubwa la zuwaru, miongoni mwa vipengele vyake ni ujumbe wa idara uliowasilishwa na muwakilishi wake Shekhe Abdulhassan Twaaiy, umeelezwa utukufu wa Bibi Maasuma (a.s), sambamba na kufungamanisha kumbukizi hiyo na mazaru ya ndugu yake Qassim (a.s).

Program unepambwa kwa qaswida zilizosomwa na Mula Husseini Karbalai.

Program hiyo ni sehemu ya juhudi za idara ya wahadhiri, zinazolenga kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na kueleza elimu na utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: