Marjaa-dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, amepongeza nakala ya kwanza ya (Msahafu wa Najafu-Ashrafu), ambayo hafla ya uzinduzi wake itafanywa siku ya Jumatano ya kesho.
Ifuatayo ni nakala ya tamko tukufu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Kila sifa njema zinamstahiki Mola wa walimwengu na rehema na Amani ziwe juu ya mbora wa viumbe, Muhammad na familia yake takatifu.
Nimefurahi kutazama katika (Msahafu wa Najafu-Ashrafu) nakala takatifu ya Qur’ani tukufu kitabu cha Mwenyezi Mungu kilichoshushwa kwa Mtume wake, ambacho ni nuru na uongofu kwa watu, kisha akakihifadhi kisibadilishwe kwa kuongeza au kupunguza kitu chochote, kitaendelea kuwa salama hadi siku ya kiyama, nacho ni hoja ya wazi na mnara wa uongofu, hakika kitabu hicho ni “Mnasihi asiyedanganya, muongozaji asiyepotosha, muongeaji asiyedanganya, hakuna mtu yeyete atakaekaa kusoma kitabu hicho ispokua ataondoka akiwa ameongeza kitu au amepungukiwa kitu, uongofu wake utaongezeka au upofu wake utapungua”.
Imepokewa kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), anasema: Namuomba Mwenyezi Mungu mtukufu kusoma kitabu chake na kutafakari aya zake pamoja na kuzifanyia kazi, hakika yeye ni mkuu muwafikishaji.
Ilihaririwa usiku wa ishirini na tatu wa mwezi wa Ramadhani mwaka elfu moja arubaini na sita hijiriyyah. Ali Husseini Sistahi.

