Kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho.. Maukibu ya watu wa Karbala imehuisha Idul-Ghadiir katika malalo ya Imamu Ali (a.s)

Maukibu ya watu wa Karbala imehuisha Idul-Ghadiir mbele ya malalo ya kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kwa kushirikiana na kitengo cha Maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Qassim Twarafi amesema: “Watu wa Karbala kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya huadhimisha Idul-Ghadiir mbele ya malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu”.

Atabatu Abbasiyya imeandaa gari 45 za kubeba zuwaru kwenda na kurudi, maadhimisho yamepambwa kwa kaswida za kidini zilizojaa shangwe na furaha katika malalo ya Imamu Ali (a.s), watu wa Karbala wamezowea kufanya maadhimisho haya matukufu katika nyoto za waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: