Mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria.. Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umeshiriki kwenye majlisi ya kumsomea dua Marjaa-Dini Shekhe Fayaadh katika mji wa Najafu

Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umeshiriki kwenye majilisi ya kumsomea dua Marjaa-Dini Ayatullah Shekhe Muhammad Is-haqa Alfayaadh (r.a) katika ukumbi wa jengo cha Alawiyya mkoani Najafu kwa muda wa siku tatu.

Majlisi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katibu mkuu Sayyid Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na baadhi ya viongozi na watumishi wa Ataba, bila kusahau kundi kubwa la walimu wa hauza, wanafunzi, viongozi wa kidini, kijamii, waumini na waombolezaji.

Wahudhuriaji wametoa salam za rambirambi kwa ndugu na wapenzi wa marehemu, wamemuomba Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi marehemu na kuwatunuku subira na utulivu wafiwa.

Marjaa-Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani ametuma salam za rambirambi kutokana na kifo cha Ayatullah Shekhe Muhammad Is-haqa Alfayaadh (r.a), akapongeza kazi kubwa aliyofanya ya kutumikia hauza na kueneza elimu ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: