Kufanya ibada ya ziara.. watumishi wa kitengo cha Baina-Haramaini wameandaa uwanja wa katikati ya haram mbili kwa ajili ya kupokea zuwaru wa siku ya Ijumaa

Wahudumu wa kitengo cha Baina-Haramaini katika Atabatu Abbasiyya wameanza kazi ya kutandika mazulia uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu na maeneo yanayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujiandaa na ibada ya ziara.

Sehemu zilizotandikwa ni pamoja na zile zenye paa, pande mbili za uwanja wa katikati na njia zinazoelekea eneo hilo, kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji wa ibada ya ziara.

Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kiutendaji unaofanywa na Atabatu Abbasiyya wakati wote, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa zuwaru na kuratibu matembezi katika eneo la katikati ya haram mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: