Muheshimiwa Sayyid Swafi amekabidhi bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amekabidhi bendera maalum ya mwezi wa Muharam mwaka 1448h ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini.

Kukabidhi bendera hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kubadilisha bendera nyekundu na kuweka nyeusi jioni ya Jumanne kama ishara ya kuanza msimu wa huzuni na uombolezaji wa msiba wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Ataba tukufu, jioni ya leo imeshuhudia ushiriki wa kundi kubwa la zuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, waliokuja katika shughuli ya kubadilisha bendera za malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ataba takatifu imefanya maandalizi makubwa, imepandisha bendera za uombolezaji kama ishara ya kupokea msimu wa huzuni mwezi wa Muharam na Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: