Katika siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam.. kitengo cha Dini kimefanya muhadhara elekezi kwa zuwaru

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa muhadhara elekezi kwa zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Muhadhara umetolewa katika siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, karibu na muda wa swala ya Dhuhuraini mbele ya kundi kubwa la zuwaru waliokuja katika malalo takatifu.

Muhadhara umetolewa na Shekhe Swalahu Karbalai, ameelezea kifo cha Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (a.s), akafafanua mafundisho yanayopatikana katika tukio hilo na akahimiza kushikamana na misingi ya harakati za Imamu Hussein na kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya.

Muhadhara huo ni sehemu ya ratiba ya kitablighi inayofanywa na kitengo cha Dini, kwa lengo la kueneza elimu ya Ahlulbait (a.s) na utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: