Kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho.. Mawakibu za watu wa Karbala zimeomboleza siku ya tatu katika mwezi wa Muharam

Mawakibu za watu wa Karbala kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya, zimeomboleza siku ya tatu katika mwezi wa Muharam, kwa kueleza matukio yaliyojiri katika ardhi ya Karbala.

Njia zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), milango yote inayoingia katika mji mkongwe hadi kwenye haram takatifu, kote kumejaa mawakibu Husseiniyya zilizokuja kuomboleza msiba huo.

Waombolezaji wamekuja kutoka maeneo tofauti ya mji wa Karbala, wakiwa wamebeba bendera za uombolezaji na kuimba tenzi za Ashura, zinazoelezea mhanga wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Kitengo kimeandaa mkakati maalum wa kuratibu mawakibu katika siku za Ashura, imehusisha upangiliaji wa matembezi ya mawakibu ili kuzuwia muingiliano baina yao na zuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: