Katika siku ya sita Muharam.. mawakibu za Karbala zinakumbuka msimamo wa wafuasi wa Imamu Hussein (a.s)

Mawakibu za watu wa Karbala kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya, katika siku ya sita Muharam, zimekumbuka msimamo wa wafuasi wa Imamu Hussein (a.s).

Njia zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), milango ya mji wa zamani hadi kwenye haram tukufu kumejaa mawakibu Husseiniyya zinazokuja kuomboleza msiba wa Karbala.

Mawakibu zimekuja kutoka maeneo tofauti ya mji wa Karbala zikiwa zimebeba bendera zinazoashiria huzuni na kuimba tenzi za kuomboleza, zinazotaja namna wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) walivyojitolea katika siku ya Ashura.

Kitengo kimeandaa mkakati maalum wa kuratibu matembezi ya mawakibu zinazokuja kuomboleza kumbukizi ya Ashura, sambamba na kubaini njia maalum kwa kila maukibu, ili kuondoa muingiliano baina ya mawakibu Husseiniyya na zuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: