Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kimetandika zulia lekundu katika eneo linalozunguka Ataba tukufu, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na ziara ya mwezi kumi Muharam.
Kazi hiyo imehusisha utandikaji wa njia zinazozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa utoaji wa huduma unaolenga kuweka mazingira mazuri kwa zuwaru wanaokuja katika mji mtukufu wa Karbala kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.
Jambo hilo ni sehemu ya ratiba ndefu inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kujiandaa na kumbukizi ya Ashura, ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu hapa katika mji wa Karbala.



