Baada ya kumaliza ziara ya Ashura.. kitengo cha Baina-Haramaini kimeanza kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili

Wahudumu wa kitengo cha Baina-Haramaini katika Atabatu Abbasiyya, wamesafishwa uwanja wa katikati ya haram mbili na sehemu ya haram tukufu baada ya kuisha kwa ziara ya Ashura.

Kazi hiyo imefanywa baada ya kuisha ziara ya mwezi kumi Muharam na nisehemu ya kujiandaa na kumbukizi ya kuzikwa miili mitakatifu ya Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake katika siku ya mwezi kumi na tatu Muharam.

Kazi hiyo imehusisha kupiga deki eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili, kwa kutumia mitambo ya kisasa na kuifanya sehemu hiyo kuwa na muonekano mzuri.

Juhudi hiyo ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu, unaolenga kuandaa mazingira mazuri ya kuendelea kupokea idadi kubwa zaidi ya zuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: