Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kimegawa sahani za chakula laki mbili na elfu thelathini na nne kwa zuwaru kuanzia mwezi kumi na moja hadi kumi na tatu Muharam.
Rais wa kitengo Sayyid Aadil Hamami amesema: “Kitengo kimegawa sahani za chakula laki mbili na elfu thelathini na nne kuanzia mwezi kumi na moja hadi kumi na tatu Muharam, kupitia mkakati wa kuhudumia zuwaru wanaokuja katika mji mtukufu wa Karbala”.
Akaongeza kuwa watumishi wa kitengo wameendelea kupika chakula na kugawa muda wote, kwa kufuata utaratibu maalum unaowezesha kufikia kundi kubwa la zuwaru.
Kitengo cha mgahawa kinagawa chakula kwa zuwaru na kuweka mazingira muwafaka kwa ajili ya kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya.


