Mkuu ya kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Karbala: Hospitali ya Alkafeel ni miongoni mwa fahari za Iraq kitiba, na kilicho ifanya iwe ya pekee inavitengo vingi na vifaa vya kisasa na uwezo mkubwa wa watumishi wake.

Maoni katika picha
Baada ya kuhudhuria katika kongamano la kwana la madaktari lililo fanywa na kitivo cha tiba (udaktari) katika chuo kikuu cha Karbala, wawakilishi wa hospitali ya Alkafeel walitoa mualiko kwa wahudhuriaji wa kongamano hilo waitembelee hospitali ya Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ili wajionee huduma zinazotolewa na hospitali hiyo na kupata maoni yao yatakayo saidia kuboresha huduma zaidi.

Ujumbe ulioenda kuitembelea hospitali hiyo ulipambwa na madaktari na wasomi wakubwa wa ndani na nje ya Iraq walioshiriki katika kongamano la madaktari, miongoni mwao ni mkuu wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Karbala dokta Riyadhi Zubaidiy ambaye baada ya kumaliza ziara yao alisema kua: “Hakika hospitali hii ni fahari kwa Iraq na kwa namna ya pekee ni fahari kubwa kwa mkoa wa Karbala, inatofautiana na hospitali zingine kwa vitengo vyake na ubora wa hutuma zinazotolewa kwa wagonjwa, hali kadhalika ina vifaa vya kisasa pia inamadaktari mahiri wanaoendana na vifaa hivyo”. Akasisitiza kua milango ya kitivo cha udaktari ipo wazi kwa kusaidiana na kushirikiana katika kuhudumia wagonjwa.

Kiongozi wa idara ya mahusiano na habari wa hospitali hii (Alkafeel) daktari Maahir Husseiniy nae alisema kua: “Ugeni umetembelea sehemu mbalimbali za hospitali na wamepewa maelezo ya huduma zinazo tolewa katika vitengo vya hospitali na wameangalia mfumo mzima wa utendaji kazi wa hospitali kuanzia kupokea mgonjwa, na wamepewa maelezo ya utendaji kazi wa vifaa vya kisasa tulivyo navyo, na mwisho wa matembezi yao wameonyesha furaha kubwa na wameiweka hospitali yetu katika ngazi za kimataifa, hakika maendeleo makubwa yaliyo fikiwa katika muda mfupi huu ni fakhari kubwa, wakasisitiza kwa wafanya kazi na watumishi wa idara kuendelea na mwenendo huu na kuongeza juhudi zaidi”.

Imetajwa kua; ugeni maalumu wa hospitali ya rufani ya Alkafeel na wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walihudhuria kongamano la mataktari la kwanza lililo endeshwa na kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Karbala, kongamano ambalo lilihudhuriwa na madaktari na wasomi mbalimbali kutoka katika vyuo vikuu vya Iraq na wengine kutoka Iran na ziliwasilishwa tafiti za kielimu zilizo lenga kuboresha kiwango cha udaktari kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: