Kitivo cha fiqhi katika mji mtukufu wa Najafu chaonyesha thamani ya mafanikio ya sekta ya Qur an katika Atabatu Abbasiyya na chafungua milango ya ushirikiano..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inaonyesha umuhimu mkubwa katika maswala ya elimu ya kiislamu na kibinadamu, pia wana mchango mkubwa katika kufanikisha miradi ya kitaaluma na wana wasiliana daima pamoja na vyuo na vituo mbalimbali vya kielimu wakizingatia kua ndio msingi muhimu wa kuangazia fikra na kupatikana kwa elimu, sekte ya Qur an imepewa umuhimu maalumu ndani ya Ataba tukufu, kimefunguliwa kitengo rasmi na kupewa jina la: “Kitengo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapa” ambacho kilichukua jukumu la kuchapisha msahafu wa kwanza hapa Iraq kwa juhudi za wairaq halisi, pia wametoa machapisho mengi ya Qur an, miongoni mwa machapisho hayo ni: Muongozo wa mwalimu, Muongozo wa mwanafunzi, mtiririko (mausua) wa visomo vya Qur an na mengineo mengi.

Mafanikio hayo ndiyo chuo kikuu cha Kufa kimeonyesha kuyathamini, hayo yalisemwa na kiongozi wa kitivo cha fiqhi, Dr. Walid Farajullah Al asadiy katika ufunguzi wa nadwa ya kielimu iliyo endeshwa na kitengo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo fanyika katika kitivo cha fiqhi, na alitanguliwa na mkuu wa kituo shekh Dhiya-u Dini Zubaidiy.

Nadwa ilifanyika siku ya (20 Desemba 2016 m) sawa na (20 Rabiul Awwal 1438 h). ya kuutambulisha mwenendo wa vizito viwili vitukufu, nao ndio mwenendo unao tegemewa katika mashindano ya Qur an yaliyo pewa jina: (Mashindano ya kitabu bora zaidi cha Qur an tukufu katika mwenendo wa vizito viwili).

Nadwa ilipata mahudhurio makubwa ya walimu na wanafunzi, kulikua na mijadala ya kielimu na michango mingi kutoka kwa washiriki, mashindano yalihusisha walimu na watafiti.

Ilielezewa hadithi ya vizito viwili na mapokezi yake hadi kutufikia pamoja na vitabu tegemezi vilivyo pokea hadithi hiyo inayo onyesha kufungamana kwa Qur an tukufu na kizazi kitukufu cha mtume (s.a.w.w).

Shekh Zubaidiy alizungumzia historia ya Qur an tukufu na riwaya zake pamoja na visomo na wasomaji, akataja pia idadi yao, kwa ujumla alielezea maarifa ya Qur an kwa kuzingatia kua ni moja ya vizito viwili, kisha akakitambulisha kizazi (itra) na wanao kusudiwa katika hadithi tukufu.

Tunapenda kufahamisha kua; Nadwa hii ilitanguliwa na nadwa zingine za kielimu kama hii zilizo fanywa na kitengo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha katika vyuo mbali mbali vya Iraq, miongo mwake ni: chuo kikuu cha Bagdad, chuo kikuu cha Mustanswariyya, chuo kikuu cha Karbala na chuo kikuu cha Basra.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: