Baada ya chuo kikuu cha Basra: Chuo cha Dhiqaar chachukua nakala za masomo ya Qur an zinazo chapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya selebasi ya masomo na kufundishia.

Maoni katika picha
Nakala za masomo ya Qur an zinazo chapishwa na kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha kilichopo katika Maahadi ya Qur an tukufu chini kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu zimeanza kuchukua nafasi kubwa, zimeanza kuenea katika uga wa kisekula ndani ya vitengo vya Qur an na masomo ya kiislamu, baada yachuo kikuu cha Basra kuviingiza rasmi katika selebasi yao ya masomo, nacho chuo cha Dhiqaar chafata nyao hizo.

Hayo yalisemwa katika nadwa iliyo endeshwa na kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dhiqaar ya kutambulisha mwenendo wa vizito viwili na mashindano ya kitabu bora cha Qur an tukufu na mwenendo wa vizito viwili pamoja na kutambulishwa kwa machapisho mengine yaliyo tolewa na kituo.

Nadwa ilipata uhudhuriaji mkubwa wa walimu na watafiti pamoja na wanafunzi, na ilitawaliwa na mijadala ya kielimu, Shekh Dhiya-u dini Zubaidiy alielezea mafanikio waliyo fikiwa katika kituo cha maarifa ya Qur an.

Pembezoni mwa nadwa hii kilifanyika kikao kilicho wahusisha kiongozi wa kitivo cha maarifa ya kiislamu. Rais wa kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha kilicha chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na ujumbe wake, katika kikao hicho walichadili kuhusu kuongeza ushirikiano katika nyanja za Qur an ili kutoa mchango katika maswala ya Qur an katika vyuo vya Iraq kikiwemo chuo cha Dhiqaar, mwishoni mwa kikao hicho Dr. Hamid Yusufu Ibrahim rais wa kitengo cha Qur an tukufu aliomba wapewe machapisho ya vitabu mengi zaidi na watavitumia kama selebasi ya kufundishia katika viwango tofauti, kama ilivyo katika chuo kikuu na Basra.

Kumbuka kua kutuo kina miradi mingi inayo husu Qur an tukufu, miongoni mwake ulikua mradi wa kuchapisha Qur an tukufu ambayo ni ya kwanza kuchapishwa hapa Iraq kwa juhudi za wairaq wenyewe katika hatua zote, pia kuna mradi wa kalamu yenye kuongea kwa Qur an tukufu na tafsiri yake na mradi wa mtiririko (mausua) wa visomo vya Qur an tukufu na yamesha kamilika majuzuu mengi hadi sasa hali kadhalika kitabu cha (muongozo wa mwalimu) na (muongozo wa mwanafunzi) na minginiyo mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: