Hospitali ya rufaa ya Alkafeel yangiza kifaa cha (Ilizarov apparatus) cha kurekebisha na kuunga mifupa..

Maoni katika picha
Miongoni mwa juhudi za kuingiza vifaa tiba vya kisasa, kiongozi kituo cha Alkafeel cha ulaya Dr. Swafaa Alhusseiniy alitangaza katia Hospitali ya rufaa ya Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kua: “Tumefanikiwa kuingiza kifaa cha (Ilizarov apparatus) cha kutibu mifupa iliyo vunjika na yenye matatizo ya kupasuka au kimaumbile, kama vile mguu mmoja kua mfupi tofauti na mwingine au kupinda kwa miguu, kifaa hiki ni miongoni mwa teknolojia ya kisasa inayo tumika katika hospitali kubwa za kimataifa.

Akaendelea kusema kua: “Utibuji wa mifupa kwa kutumia kifaa hiki, hufanyika kwanza upasuaji na kuangaliwa sehemu yenye tatizo katika mfupa kisha huwekwa kitu ambacho kitaufanya mfupa uwe kama wa mtoto unao endelea kukua, na ukuaji huo unaelekezwa kwa namna ya tatizo lilivyo halafu anavaa kifaa kinacho zuia mguu kwa nje, unaweza kupangilia utakavyo namna ya ukuaji wa mfupa bila kupasuliwa tena, kisha baada ya kupona anatolewa kifaa alicho fungwa kwa nje”. Akabainisha kua: “Kifaa hiki hutumika kwa kuunganisha sehemu iliyo pasuka, kurekebisha sehemu za maungio, kurefusha mifupa, kuurejesha mfupa mahala pake uliotoka kutokana na jeraha, na kurekebisha matatizo ya mifupa”.

Naye daktari wa kirusu; Alexander Mitrovanov anaye patikana katika hospitali ya Alkafeel alisema kua: “Hakika kifaa hiki ni miongoni mwa vifaa vya kisasa katika tiba ya mifupa, kina uwezo wa kuongeza ulefu wa mfupa kwa kati ya (cm, 15 hadi cm, 30) na hutumika na kifaa saidizi kinacho fungwa kwa nje”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali tembelea (www.kh.iq) au piga simu: (07602344444) au (07602329999) na kwa maelezo kuhusu kituo cha ulaya piga simu: (0780216989).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: