Kitengo cha uhandisi chakarabati milango ya uwanja wa haramu ya Abulfadhili Abbasi (a,s)..

Maoni katika picha
Kitengo cha uhandisi ndani ya siku hizi kimekua na kazi nyingi za kukarabati maeneo mbali mbali ya Ataba tukufu ndani na nje ya haramu tukufu, kutokana na ratiba ya kazi iliyo wekwa na kitengo, ukarabati huu unafanyika bila kuathiri watu wanaokuja kufanya ziara wala kuathiri ratiba za watumishi wengine wa Ataba tukufu, leo tumeangazia moja ya kazi ya kurekebisha milango ya uwanja wa haramu tukufu na kuifanya iwe rahisi kuingia na kutoka kwa watu, imeongezwa urefu kwa nje na kwa ndani.

Kazi hii itahusisha milango yote ya haramu tukufu, baada ya kukamilika kazi ya kuiwekea marumaru kwa nje miongoni mwa kazi za upanuzi wa Haramu, kitengo chetu kitachukua jukumu la kurekebisha milango kwa kuweka marumaru chini ya milango kuanzia usawa wa milango ya zamani hadi upande wa ndani ya haramu, kwa sasa kazi inaendelea katika milango mitatu ambayo ni: mlango wa Qibla na mlango wa imam Mussa Alkadhim pamoja na mlango wa imam Ali Alhaadi (a.s), na itaendelea katika milango yote, pia itabadilishwa sakafu ya chini ya milango kutokana na vipimo vilivyo kwisha fanywa, na itawekwa sehemu maalumu katika kila mlango ya kupita watu wenye ulemavu wa viungo hususan wale wanaotumia kiti cha mataili, na hasa katika mlango wa Qibla, kwa sababu huu ndio mlango mkubwa zaidi ya milango mingine yote ya Ataba tukufu.

Ikumbukwe kua ofisi ya uanzilishi iliyopo chini ya kitengo cha uhandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa ofisi muhimu, kutokana na majukumu iliyo nayo ndani na nje ya Ataba kwani ofisi hii ndiyo hufanya tathmini na upembuzi yakinifu kisha huingia katika utekelezaji na kufatilia ukamilifu wa jambo husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: