Hakika wizara ya malezi inajivunia uwepo wa shule za Abulfadhili Abbasi (a.s), na inatamani kuwe na ushirikiano kati ya wizara na shule hizi, hakika tumekuta mazingira bora ya kielimu ambayo ni nadra kuyakuta hapa Karbala na Iraq kwa ujumla, na haya ni mafanikio makubwa kwa raia wote wa Iraq.
Akaendelea kusema kua: “tumetembelea shule kadhaa za Abulfadhili Abbasi (a.s) kuangalia mazingira ya kielimu na kimalezi, na tumekagua madarasa na vifaa vya kufundishia, tumekuta mazingira yanayo furahisha sana, hakika yanaendana na utukufu wa mji wa Karbala, miongoni mwa tuliyo kuta ni, kukamilika kwa vifaa muhimu vyote, na mazingira bora ya masomo, na uwezo mkubwa wa walimu, ikiwemo umakini mkubwa wa idara katika utendaji wao”.
Akaendelea kusema kua: “Hakika shule za Abulfadhili Abbsi (a.s) zinatoa ushindani mkubwa wa kimaendelea kwa shule za serikali na shule binafsi zingine, natoa wito kwao waje kutembelea shule hizi kwani kushindana katika maendeleo ni jambo zuri, shule za serikali na binafsi zijaribu kuiga kutoka katika shule hizi za Abulfadhili Abbasi (a.s) ambazo zimepiga hatua kubwa”.
Kumbuka kua ziara ilihusisha (shule ya msingi Al ameed ya wasichana, shule ya msingi Assaaqi ya wavulana na shule ya awali ya Assaaqi), ugeni uliangalia wanafuni na njia za ufundishaji, pia waliangalia ratiba za masomo.
Katika matembezi yao walifatana na kiongozi wa shule binafsi na mkuu wa kitengo cha malezi katika mji wa Karbala tukufu, Ustadhi Ikhlasi Abdulqaadir Asadiy, na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Al ameed ya wasichana Ustadhat Minna Wailiy ambaye alitoa maelezo kamili kuhusu mazingira ya malezi na elimu katika shule hizo.