Mtandao wa Alkafeel wa kimataifa waingiza mtandao mpya wa lugha ya Kiswahili

Maoni katika picha
Idara ya intanet iliyo chini ya kitengo cha habari na utamatuni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuingizwa kwa mtandao wa lugha ya Kiswahili, ambayo imeongezwa katika mitandao yake mingine ya lugha za: (Kiengereza, Kifarsi, Kituruki, Kiurdu na Kifaransa) ukiongeza lugha ya kiarabu. Hivyo mtandao huu utakua ni moja ya njia za kuwafanya wakazi wa nchi za Afrika Mashariki wanufaike na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kila anaye fahamu Kiswahili katika miji mingine, hii ni kutokana na umuhimu wa kufunguka katika nyanja ya mawasiliano na mataifa mbali mbali.

Mtandao huu umekuja kutokana na haja kubwa ya kuitambulisha Atabatu Abbasiyya tukufu na kuifanya iweze kufika kila kona ya Dunia, unaendeshwa na watu waliobobea, na unakurasa nyingi, kama vile: Harari, Ziara kwa niaba, Maonyesho ya picha, Mambo yanayo onekana na Khutuba za swala za Ijumaa ikiwepo Miradi ya Ataba tukufu, kulingana na mada zinazo endana na mtandao huu.

Kuhusu kupangiliwa kwake, wataalamu wa idara ya Intanet wametumia njia bora kabisa katika kuipangilia, kama walivyo weka njia rahisi ya kuwasiliana na watu wanaofanya kazi katika mitandao. Unaweza kutembelea mtandao mpya wa Kiswahili kupitia anuani hii: https://alkafeel.net/?lang=sw

Kumbuka kua asili ya lugha ya Kiswahili, ni lugha ya watu wa fukwe za Afrika Mashariki na inazungumzwa zaidi Kenya na Tanzania, na inazungumzwa na zaidi ya watu miloni hamsini na tano pia ni miongoni mwa lugha za kibantu, lakini imeathiriwa zaidi na maneno ya kiarabu, kiasi kwamba inamaneno mengi ya kiarabu pia kireno kwa sasa inaandikwa kwa herufi za kilatini lakini hapo awali ilikua inaandikwa kwa herufi za kiarabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: