Hatua kubwa imepigwa na idara ya ukarabati na uwekaji wa maraya katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Mafundi wanaendelea na ukarabati na uwekaji wa Maraya (marumaru za vioo) katika haramu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuondoa maraya mbovu na kuweka mpya zenye rangi na nakshi nzuri, mara ya mwisho kazi hii imefanywa katika upande wa mlango wa kichwa kitukufu na kazi imekamilika kwa asimilia (%50) takriban, kazi hii inafanywa na idara ya maraya iliyo chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbaiyya tukufu.

Kuhusu kazi hizi kiongozi wa idara ya Maraya aliiambia Alkafeel kua: “Kazi ya kurepea Maraya katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inaendelea vizuri, baada ya kukamilika katika upande wa mlango wa imamu Muhammad Jawaad (a.s) hadi katika upande wa mlango wa imamu Mussa Kaadhim (a.s) tumeweka maraya zenye rangi pamoja na marekebisho mengine yaliyo jitokeza, na tumeanza kazi katika upande wa mlango wa kichwa kitukufu ambapo tumesha kamilisha kiasi cha asilimia (%50) takriban, na tunatarajia kukamilisha ndani ya mwezi mmoja inshallah”.

Akaendelea kusema kua: “Kama kawaida, tumetoa maraya zilizo haribuka na kutengeneza sehemu zenye ufa kwa kutumia (BRC) kisha tukaweka chokaa na jibsu ili (ukuta) uwe imara zaidi na uweze kubeba maraya vizuri, ama kuhuru taa za mapambo (disco light) zilizo wekwa hivi karibuni ambazo zipo katika umbo la nyota, tumezifanyia baadhi ya marekebisho, tumezizungushia duara ya alminiam ilikuziimarisha na kuzipendezesha, duara la zamani lilitengenezwa kwa chuma”.

Kuhusu kazi za Maraya zilizo kamilika hadi sasa alisema kua: “Kazi iliyo kamilika hadi sasa ni nusu duara zilizopo upande wa mlango wa Furat (Alqamiy) na mlango wa imam Muhammad Jawaad (a.s) hali kadhalika maandishi ya Qur an yaliyopo katika kubba tukufu hadi chini ya duara zinazo zunguka malalo matukufu, pia kutoka katika mlango wa Sat-hul Haram hadi katika mlango wa Ummul banina na kazi inaendelea hadi tumalize kuweka maraya katika haram yote inshallah”.

Tunapenda kukumbusha kua; Idara ya Maraya inaendelea na kazi ya kubadilisha maraya katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kutoa maraya zilizo haribika na kuweka mpya zenye rangi nzuri zinazo endana na sehemu husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: