Fahamu vifaa vilivyopo katika makumbusho ya Alkafeel miongoni mwa vitabu kale na zana za kivita za zamani..

Maoni katika picha
Miongoni mwa makumbusho za kwanza kufunguliwa katika Ataba za Iraq ni makumbusho ya Alkafeel ya vifaa (zana) na vitabu kale iliyopo ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo ilifunguliwa mwaka wa (2009 m) katika kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), makumbusho yana idadi kubwa ya vifaa vya kihistoria, baadhi yake vina mamia ya miaka na miongoni mwa vifaa hivyo ni zana za kivita za zamani, kama vile; majambia, mapanga, sime nk. Vinarejea katika historia ya miaka tofauti, baadhi yake kabla ya ufalume na baadhi tulivipata kutoka kwa mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika zama tofauti.

Mtandao wa Alkafeel ulikutana na kiongozi wa makumbusho ustadhi Swadiq Laazim kutaka kufahamu zaidi kuhusu panga (zana za kivita) akatuambia kua: “Makumbusho ya Alkafeel ina idadi kubwa ya panga, jambia na sime, na sababu ya jambo hili ni kwakua Abulfadhil Abbasi (a.s) alikua ni kiongozi wa jeshi la ndugu yake imam Hussein (a.s), na huchukuliwa kua alama ya ushujaa na kujitolea na alikua mwanaume wa shoka (shujaa), hivyo viongozi na mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) wanaona fahari kwao kutoa zawadi ya vifaa vyao vya kivita na kuviweka katika makumbusho haya matukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa hiyo zana zilizopo katika makumbusho ya Alkafeel na stoo zake ni nadra kuzikuta katika makumbusho mengine za Ataba.

Tuna idadi kubwa ya panga, jambia na sime na vifaa vingine nadra, ambavyo vinarudi katika vipindi tofauti, sehemu ya vifaa hivyo ni zawadi kutoka kwa wafalume na watawala wa miji tofauti na katika zama tofauti, na vingi vimetengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu, miongoni mwa vifaa hivyo ni panga la Sultani wa utawala wa Othumaniyya Salim Khaan, na upanga wa Sultani Zandi Jafari Kahaan Zandi na panga la Sultani Qaajari Fat hu Ali Shaha, asilimia kubwa ya panga hizo zina naksi na maandishi ya dhahabu”.

Akaendelea kusema kua: “Panga zilizopo katika makumbusho utengenezwaji wake unarudi katika karne za nyuma, huenda upanga wa nyuma zaidi ukawa na zaidi ya miaka (500), panga hizi mara nyingi zemetengenezwa kwa madini tofauti, huchukuliwa kua ni zana za thamani, na zimetengenezwa kwa umaridadi mkubwa, ni nyembamba na kali sana, huku upande wa mpini (kushikia) ukiwa umetendenezwa kwa pembe za swala, nyumbu au wanyama wengine, pia makumbusho inavifaa vya aina ya shoka, ambavyo mpiganaji anayetumia farasi huweka katika farasi yake wakati wa vita pia kuna ngao zilizo tengenezwa kwa chuma na zingine kwa mbao huku zingine zikiwa zimetengenezwa kwa ngozi na kunakshiwa kwa herufi na alama nzuri”.

Kuhusu utunzaji na uhifadhi wa vifaa hivi alisema kua: “Vifaa hivi husafishwa kwa namna maalumu ya kusafisha vifaa kale, ukizingatia kua watumishi wa makumbusho wana ujuzi mkubwa na wanavyeti vya fani hizi, na utunzaji wetu ni salama zaidi, hutunzwa kwa kiwango cha joto na baridi maalumu, pia kuna namna ya kutunza kifaa kwa kutumia plastick, njia hii inatumika kutunzia panga na vifaa vingine vya kivita inakua rahisi kutoa na kurudisha kifaa mahala pake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: