Sayyid Ahmadi Swafi alipo kutana na jopo la wataalamu wa ki Iraq: Iraq ni nchi yenye watu wenye vipaji pamoja na mapungufu ya serikali ya kuto wajali sisi tupo tayali kuwalea.

Sehemu ya kikao
Kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amezungumza na jopo la wanazuoni wa ki Iraq waliopo chini ya tume ya wataalamu wa Iraq akasema: “Tumejaribu kufanya kua siasa ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni kutilia umuhimu swala la kutegemea vipai na vipawa vya wairaq katika kutekeleza miradi yetu mbali mbali”. Akaendelea kusema kua: “Mimi naamini kua wairaq wana akili ya ubunifu na fikra pevu, wanahitajia mtu wa kulea fikra hizo na kuzifasiri katika uhalisia, kuzifanyia kazi sio kwa maneno, ni kwa vitendo, na ni jukumu la mwenye kusaidia kua na uvumilivu pamoja na kustahamili makosa ya kiutendaji yanayo weza kutokea kwa bahati mbaya, pindi inapotokea kosa la bahati mbaya na likapelekea kufeli kwa mradi, inabidi mfadhili asimame pamoja na mtaalamu na kumpa nafasi nyingine ili asahihishe kosa lake, na hivi ndio Ataba inavyo fanya kazi, kwanza inajali kutumia muda vizuri na kuongeza vipawa na uwezo wa wataalamu”.

Akaendelea kusema kua: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu, uzoefu wetu umefaulu, na miradi imekamilika kama ilivyo pangwa, ushahidi tunao, miongoni mwake ni kiwanda cha mbolea kinacho fanya kazi chini ya usimamizi wa dokta Ali Bahadali”. Kisha akasema: “Mimi nafarijika sana na uwepo wenu, hakika sisi tunathamini sana uwezo na vipawa vyenu pia sitaki mkate tamaa kutokana na yanayo jiri hapa nchini”.

Akafafanua kua: “Sisi tuna wabunifu wengi, tunajitahidi kuwatengenezea mazingira mazuri na kuhakikisha wanapata riziki zinazo endana na elimu zao, kwani iwapo wakitelekezwa ubunifu wao utakufa, na hilo jambo hatutaki kuliona”.

Akaongeza kua: “Sisi tupo katika nchi ambayo, serikali yetu mara nyingi haitumii watu wenye vipawa vya ubunifu, hasa ndani ya miaka kumi na tatu iliyo pita, watu wenye vipawa wamepuuzwa na wametengwa, na hasa ilipo anza kushughulishwa na vita vya magaidi inayo endelea hadi sasa, watu wengi wenye vipawa wamehama nchi na wameenda kufanya kazi nchi za nje na huko wana mchango mkubwa sana, nchi hizo ninaneemeka kutokana na uwezo wao wa kiakili na ikhlasi katika utendaji wao, pamoja na hayo yote Iraq ni nchi yenye watu wenye vipaji”.

Halafu akawaambia kua: “Linaweza kufanywa kongamano la wairaq wenye vipaji, na Atabatu Abbasiyya tukufu ipo tayali kuliendesha, lipangiliwe vizuri, lihusu ubunifu katika maswala ya viwanda mbali mbali”.

Akaongeza kua: “Inatakiwa lifanyike kongamano na maonyesho ya kimataifa, hatuna kizuizi cha kuunda kamati ya wataalamu ya Ataba tukufu ikashirikiana pamoja na nyie kwa ajili ya kuratibu swala hili na mkakubaliana katika mambo ya msingi, sio vibaya mkifanya vikao vya mara kwa mara au warsha kwa ajili ya kuhakikisha swala hili linafanyika katika hali nzuri”.

Sayyid Swafi akabainisha kua: “Hakika nchi yetu ilikua na uwezo wa kupata maendelea bora ya haraka tofauti na ilivyo sasa, kama kungekua kuna wanaosikiliza tunayo waambia, lakini mwafahamu sauti zetu zinapuuzwa hakuna yeyote anaye tusikiliza”.

Kumbuka kua kikao hiki kilitokana na ziara iliyo fanywa na ugeni wa wabunifu wa ki Iraq katika Atabatu Abbasiyya tukufu, walitembelea miradi mbali mbali ikiwemo, Daarul Kafeel, mradi wa uchapaji na usambazaji, na Mazaariu Khairaat (mashamba) ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: