Chuo cha masomo ya kibinadamu chafanya mtihani wa hatua ya pili katika lugha la kifarsi na chasisitiza kuendelea na kozi hii..

Sehemu ya mtihani
Baada ya kumaliza kozi maalumu ya lugha ya kifarsi kwa wasiozungumza kifarsi ambayo wataenda kuimalizia Iran, kitengo cha lugha katika chuo cha masomo ya kibinadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa mtihani wa awamu ya pili wa lugha ya kifarsi, na huu ni mtihani wa pili kufanyika ndani ya Iraq na nje ya Iran.

Washiriki wa mtihani walikua wanafunzi (19) miongoni mwao wanafunzi (14) wamefanya mtihani wa hatua ya nne na tano, huku wanafunzi (5) wakiwa wamesoma katika kozi inayo endeshwa na kitengo cha utamaduni wa Iran katika mji wa Bagdad, na wamepewa vyeti vya kuhitimu kozi hizi, vyeti hivi vinakubalika kwa sababu idara ya lugha ndio muwakilishi pekee wa kituo cha kimataifa cha kufundisha lugha ya kifarsi katika chuo kikuu cha Fardusy kilichopo Mash hadi huko Iran, hutoa kozi za kifarsi katika shule za kisekula na kutoa mitihani katika mikoa tisa hapa Iraq, kutokana na makubaliono kati ya chuo cha masomo ya kibinadamu na kituo cha kimataifa cha kufundisha lugha ya kifarsi katika chuo kikuu cha Fardusiy huko Mash hadi.

Katika mtihani huu pia alihudhuria dokta Abbasi Didda rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu na dokta Jaasim Ibrahimiy na dokta Swafaau Abduljabaar Ally Mussawiy mkuu wa kitivo cha masomo ya kibinadamu pamoja na kiongozi wa idara ya lugha ustadh Muhammad Swabaar ambaye alisema kua; idara inaendelea na kutoa kozi hii na inatarajia kuongeza na lugha zingine.

Kumbuka kua washiriki walihudhuria masomo kwa muda wa miezi sita, masaa (440) ya masomo wamesomeshwa mambo yote ya lazima katika lugha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: