Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea na ratiba yake ya kusaidia familia za mashahidi na majeruhi wa Hashdi Sha’abiy..

Maoni katika picha
Toka siku za kwanza ilipo tolewa fatwa tukufu ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, Atabatu Abbasiyya tukufu imebeba majukumu mengi, yanayo lenga kuwasaidia wapiganaji, katika viwanja vya vita au kwa kuwasiliana na familia za mashahidi na majeruhi, yote haya ni sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Marjaa dini mkuu, yanayo sisitiza kuwasaidia wapiganaji na kuwajengea mazingira yatakayo wapa nguvu zaidi ya kuendelea kupigana na magaidi wa kidaesh, Atabatu Abbasiyya tukufu imesha toa misaada mingi kwa wapiganaji na familia za mashahidi na majeruhi bila kuangalia itikadi wala mielekeo yao, miongoni mwa kutekeleza swala hilo, kitengo cha mahusiano kwa kusaidiana na kitengo cha dini pamoja na kitengo cha habari na utamaduni wamefanya ziara hii ya kuwatembelea familia za mashahidi na majeruhi wa Hashdi Sha’abiy na kuwapa misaada ya kimadda na kimaanawiyya pamoja na tabaruku kutokana na ratiba ilivyo pangwa, ziara hii imefanywa kwa kuratibiwa na Mu’utamad Marjiiyya dini mkuu katika miji hii.

Kwa ajili ya kufahamu zaidi kuhusu msafara huu tumeongea na mjumbe wa msafara Ustadh Rasuul Naaji kutoka katika kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye alisema kua: “Ratiba hii imepewa baraka na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), tumejiandaa kutembelea familia za mashahidi na majeruhi wa Hashdi Sha’abiy na kuchangia kuwasaidia, kwani wameihami Iraq na maeneo yake matukufu kwa roho zao, wamejitolea kwa ajili ya nchi hii, tumekutana na familia za mashahidi na tukawapa misaada pamoja na tabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na tunajitahidi kusimama pamoja nao katika haja zao, hii ni sehemu ndogo sana ukilinganisha na namna wao walivyo jitolea, hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya hivi mfululizo ili kuzifanya familia za mashahidi wahisi kua kuna watu wanao wajali na kuthamini mchango wao na ushindi mkubwa unao patikana kutokana na damu za watoto wao, ziara hii imehusisha mji wa Basra, na tumegawa zawadi kwa familia (300) za mashahidi na majeruhi, katika eneo la mjini na kitongoji cha Qarna pamoja na kitongoji cha Abu Khaswaibu kikiwemo pia kitongoji cha Albushawi pamoja na Hawiir”.

Naye Shekh Aadil Wakiil, makamo rais wa kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye ndiye mkuu wa msafara alisema kua: “Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu tumekuja na zawadi ndogo tunazo wapa familia za mashahidi, ninapo sema ndogo, ni kwa sababu hakuna unacho weza kumlipa shahidi kutokana na utukufu wake, hivyo tumekuja na zawadi tunazo wapa familia za mashahidi ambao wamejitolea kuihami Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu, familia za mashahidi wanaona utukufu na fahari kwao kwa kupatikana mashahidi katika familia zao kwa ajili ya kuihami Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu, lakini wanahitaji zaidi kuendelea kuwasiliana nao”.

Familia za majeruhi wameonyesha kuridhika kwao na hukumu ya Mwenyezi Mungu, na wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kuwakumbuka na kuwapatia misaada hii inawafanya wajihisi kua kuna watu wanao wajali na kuwakumbuka.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu ya kutoa misaada ya lazima kwa familia za mashahidi na majeruhi, wameandaa ratiba kamili ya kuwatembelea mfululizo familia za mashahidi na majeruhi katika miji yote ya Iraq, kwa ajili ya kuwajulia hali na kuwapa misaada stahili kutokana na kujitolea kwa watoto wao, ziara hizi zinaendelea hadi tuzifikie familia zote za majeruhi na mashahidi kuanzia kutolewa kwa fatwa ya jihati ya kujilinda tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: