Kongamano hili linalenga mambo yafuatayo:
Kwanza: Kuutambulisha mkoa kijamii na kitamaduni.
Pili: Kusaidia taasisi za kidini kuanzisha makumbusho za kisasa na kuendeleza fani za makumbusho.
Tatu: Kuanzisha uhusiano na taasisi zinazo simamia makumbusho za kitaifa na kimataifa.
Nne: Kuongeza uwelewa kuhusu faida za makumbusho kijamii na kiuchumi kupitia vyombo vya habari.
Mada zitakazo wasilishwa katika kongamano ni:
- 1- Elimu kuhusu makumbusho.
- 2- Misingi ya kielimu inayo tumika kimataifa kuzitambua makumbusho.
- 3- Mikataba na sheria za kimataifa kuhusu kuzihami makumbusho.
- 4- Njia za kisasa zinazo tumika katika kulinda na kukarabati makumbusho.
- 5- Njia za kitaalamu katika maonyesho ya makumbusho na vigezo vyake.
- 6- Manufaa ya makumbusho na athari yake katika uchumi wa nchi.
- 7- Mawasiliano ya vyombo vya habari katika kuelezea tamaduni za makumbusho.
Tumeunda kamati ya wataalamu itakayo simamia swala hili, inayo jumuisha wasomi na watafiti wa kisekula, bila shaka washiriki watatoa tafiti zao zitakazo onyesha njia bora za kushirikiana baina ya makumbusho na nchi zitakazo shiriki katika kongamano, na namna ya kuifanya makumbusho ionyeshe uwepo wake katika jamii, pia wataonyesha maendeleo ya makumbusho zingine kiteknolojia na njia za kutunza makumbusho na kuifanya iweze kumuathiri mtu anaye kuja kuitembelea, pia tutaangalia nafasi za wakuu wa makumbusho, watafiti na wasomi.