Kuanza kwa maandalizi ya awamu ya pili ya mashindano ya fani ya kuhutubu kwa wanafunzi wa shule za upili (sekondari)..

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio yaliyo patikana katika awamu ya kwanza ya mashindano ya fani ya kuhutubu kwa wanafunzi wa shule za upili (sekondari), ofisi ya harakati za kishule chini ya idara ya mahusiano na vyuo vikuu iliyo chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza maandalizi ya kufanya awamu ya pili ya mashindano hayo, yanayo tarajiwa kufanyika ndani ya mwezi wa tatu ujao.

Mashindano haya ni sehemu ya harakati za mradi wa Alkafeel mzalendo unao endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, mada zitahusu mambo mawili muhimu, ambayo ni; kuipenda nchi na kuunga mkono jeshi na hashdi sha’abi pamoja na mafanikio wanayo pata dhidi ya magaidi ya kidaesh, mashindano yatadumu kwa siku mbili, siku ya kwanza kutakua na vipindi vya asubuhi na jioni huku siku ya pili kutakua na hafla ya kufunga mashindano na kutangazwa majina ya washindi.

Baada ya kuainisha mada zitakazo shindaniwa, kamati ya maandalizi imetoa mialiko katika vituo vya malezi vya mkoa wa Waasitu na Junubu kwa ajili ya kuandaa wanafunzi watakao shiriki, ambao huteuliwa na shule zao kama ilivyo fanyika mara ya kwanza, wanafunzi hao watapambana kwa kuzungumza (kutoa khutuba), kutakua na majaji ambao watachagua washindi watano miongoni mwa washiriki.

Kumbuka kua; awamu ya kwanza ilikua na washiriki (45) waliotoka katika shule za miji mbali mbali (Karbala tukufu, Najafu tukufu, Bagdad, Muthana, waasitu, Basra, Baabil, Dhiqaar, na Qaadisiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: