Mradi wa nyuki (mizinga) ni moja ya miradi iliyopo katika sekta ya kilimo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa juhudi za kuingiza kipato cha ndani, na kuongeza pato la kilimo, pia kujenga uwezo wa kujitosheleza kwa mkoa wa Karbala katika mazao ya nyuki.
Wataalamu wa mradi wa nyuki wamefanya juhudi kubwa na wamepata matokeo chanya (mazuri) kwa kuzalisha asali nyingi iliyo zidi ile iliyozalishwa mwaka (2015), ndani ya mwaka uliopita (2016) kwa mujibu wa mkuu wa idara ya nyuki mtaalamu wa kilimo Hussein Muhammad Abduridha alisema kua: “Hakika tumezalisha kiasi cha (3500 kg) za aina mbali mbali za asali kutokana na mahitaji, pia tumeotesha mimea mingine ambayo husaidia kupata aina tofauti za asali, kwa sababu nyuki hutegemea mimea na mauwa katika kutengeneza asali, pia tumezalisha nta ambayo hutumika katika kutibu maradhi mengi moja kwa moja au kwa kuchanganywa na vitu vingine”.
Akaendelea kusema kua: “Bidhaa zetu zinapendwa na zimekubalika sana ndani na nje ya Iraq, kwa sababu zinazalishwa katika sehemu inayo aminika, ni asali halisi na safi (%100) kwa mujibu wa tafiti za wataalamu, kwa sababu nyuki wetu hatuwalishi maji na sukari kama vinavyo fanya vituo vingi vya ufugaji wa nyuki hivi sasa”.
Akaendelea kusema kua: “Zoezi letu la upandikizaji wa nyuki wa asili wanao tengeneza asali nyingi limefanikisha, pia tumeingiza kizazi kipya cha nyuki wa asili wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza asali, mfano wa nyuki wa Itali, pia tunazalisha asali tiba kutokana na mimea tiba”.
Kwa maelezo zaidi ya mradi wa nyuki, unaweza kutembelea kituo chetu kilichopo katika mji wa Karbala (vitalu vya Alkafeel) katika barabara ya Husseiniyya, au kituo cha pili kilichopo katika mji wa Najafu barabara ya Jaamia. Pia unaweza kupiga simu kwa namba zifuatazo: (07712446430) au (07718003738).