Pointi muhimu katika vyakula: Maudhui ya semina iliyo endeshwa na kitengo cha mipango na maendelea ya binadamu..

Maoni katika picha
Kitengo cha mipango na maendeleo ya kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha semina yenye anuani isemayo (pointi muhimu katika vyakula) kwa watumishi wa Ataba wanao fanya kazi katika idara ya chakula kwa kufata taratibu za kimataifa (Haasib).

Haasib ni utaratibu wa kuangalia usalama wa chakula, kupitia utaratibu huo unaweza kubaini hatari zinazo tishia ubora wa chakula.

Semina hii ni miongoni mwa semina nyingi zinazo tolewa na kitengo hicho kwa watumishi wa Ataba ili kuongeza uwezo wa watumishi katika kutekeleza majukumu yao.

Msimamizi mkuu wa semina hii, muwezeshaji wa kimataifa Ustadh Jafari Mansuur ambaye ni mshauri mkuu wa mafunzo ya kimataifa katika mamlaka ya Baharaini aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika semina hii tumeangalia utaratibu wa (Haasib) na hatua za maendelea yake, hii ni miongoni mwa njia zinazo tumika sana katika uandaaji wa chakula, utaratibu huu unafungamana na taratibu zingine zinazo lenga kutoa chakula kinacho linda afya na salama hususan kwa watu wanaokuja kuzuru malalo ya Abulfadhi Abbasi (a.s) wanapo tabaruku kwa kupata chakula katika mudhifu (mgahawa wa hapa ndani). Na namna ya kuhifadhi nafaka za chakula na kuzipika pamoja na kukipanga kwa walaji, na njia ambazo hutumika mara nyingi katika upangaji wa chakula, pia tuliangalia usafi binafsi (wa wahudumu) na umuhimu wake katika kulinda usafi wa chakula”.

Akaendelea kusema kua: “Utaratibu huu unaanzaia katika kuhifadhi chakula (stoo) kukipika na kukipeleka mbele ya mlaji (zaairu wa Ataba tukufu), na unalenga kuongeza uelewa wa kiafya kwa watumishi, hakika utaratibu huu ni mzuri sana katika kulinda watu kutokana na sumu za vyakula ambozo hupatikana kikemia, fizikiya au baiolojia, na hubaini pointi muhimu za kuzingatia kwa ajili ya usalama wa watu”.

Akabainisha kua: “Idadi ya washiriki wa semina hii ambayo imedumu kwa siku tatu walikua watumishi (14) kutoka katika idara tofauti vya Ataba tukufu, washiriki wote wameifurahia sana semina hii na wametambua umuhimu wa kuufanyia kazi utaratibu huu”.

Tunapenda kusema kua; kitengo cha mipango ya maendeleo ya binadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo hai, huendesha semina za kujenga uwezo mara kwa mara kwa watumishi na kuendeleza taaluma zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: