Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza ratiba ya umra kwa familia za mashahidi na majeruhi wa hashdi sha’abi..

Maoni katika picha
Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza ratiba ya msafara wa saaqi wa kwenda kutekeleza ibada ya umra na kuzuru kaburi la mtume (s.a.w.w) na maimamu wa Baqii (a.s) na sehemu zingine takatifu katika mji wa Maka na Madina kwa punguzo la bei kwa ajili ya familia za mashahidi na majeruhi wa hashdi sha’abi, ikiwa kama sehemu ya kusaidia familia hizo tukufu na kuwakirimu ndugu zao ambao wamejitolea damu na roho zao kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo yake matakatifu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Dhiyaau Dini alisema kua ni pamoja na:

  1. Viza.
  2. Makazi siku nne Madina na siku sita katika mji wa Maka takatifu.
  3. Kutembelea maeneo matukufu katika mji wa Madina na Maka.
  4. Usafiri wa Madina na Maka pamoja na ule wa kutoka na kurudi katika uwanja wa ndege wa Jida.

Siku ya kwanza: kukutana katika garage (maegesho ya magari) ya Saaqi katika barabara ya Maitham Tamaar na kwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya Jida, baada ya kufika Jida tutaenda Madina na kugawa vyumba katika moja ya hoteli za Madina.

Siku ya pili: kuzuru msikiti mtukufu wa mtume, kama muda ukitosha tutazuru maimamu wa Baqii (a.s) kisha utakua muda wa kupumzika.

Siku ya tatu: kuzuri maeneo matukufu ya Madina (Mashahidi wa Uhudi, Masjid Qiblataini, Misikiti saba na Masjid Kuba).

Siku ya nne: kupumzika (hakuna ratiba).

Siku ta tano: muda wa kupumzika, baada ya adhuhuri tutaondoka na kuelekea katika mji wa Maka mtukufu, baada ya kufika huko vitagawa vyumba vya kulala.

Siku ya sita: kutekeleza ibada ya Umra.

Siku ya saba: kupumzika (hakuna ratiba).

Siku ya nane: kuzuru maeneo matukufu ya Maka (Mlima Thuur, Mlima wa Arafaat, Muzdalifa, Mina, Mlima Noor na makaburi ya Hajuun).

Siku ya tisa: kufanya Umra kwa niaba kwa wale watakao penda kufanya hivyo.

Siku ya kumi: kupumzika (hakuna ratiba).

Siku ya kumi na moja: kurudi katika nchi yetu kipenzi na kufika na elufu salama.

Fahamu kua gharama ya kushiriki katika safari hii kwa mtu mmoja; keshi ni ($800) na kwa mkopo ni ($825) na mtoto kuanzia miaka 2 hadi 11 ni ($500) keshi na mkopo ni ($525) na mtoto anaye nyonya mwenye umri chini ya miaka miwili ni ($250) keshi na mkopo ni ($275).

Kwa anaye taka kukopa ni lazima adhaminiwe na mfanya kazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kiwango atakacho kopeshwa kitakatwa katika mshahara wa mfanyakazi huyo kila mwezi, na atatakiwa kutanguliza ($200) na kiwango kitakacho bakia kitakatwa ($100) katika kila mwezi kutoka katika mshahara, na anaye kopa kwa ajili ya mtoto mwenye umri wa miaka 2 hadi 11 atatanguliza ($100) na itakatwa ($100) kutoka katika mshahara kila mwezi.

Mtu anaye taka kwenda Umra anatakiwa awasilishe paspoti yake na iwe ina zaidi ya miezi sita ya muda wa kuendelea kutumika kwake, pamoja na kitambulisho chake na picha tatu za paspoti size zenye barck ground nyeupe kwa ajili ya kumuandaliwa viza: kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyopo katika mlango wa Bagdadi –jengo la imamu Hassan Askariy (a.s)- hoteli Dallah ya zamani, au unaweza kupiga simu kwa namba zifuatazo:

(07602283026) au (07801952436).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: