Kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu: shirika la Cement la Iraq lawakirimu zaidi ya familia mia moja za mashahidi..

Maoni katika picha
Ukumbi wa imamu Hassan (a.s) uliopo ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo (1 Jamadil Ula 1438h) sawa na (30 Januari 2017m) kumefanyika kongamano la hafla ya kuwakirimu zaidi ya familia mia moja za mashahidi wa jeshi na hashdi sha’abi katika mkoa wa Karbala tukufu.

Hafla imefanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Nyie ni fahari kwetu na utukufu wetu lau si nyie isingepandishwa bendera), hafka hii imefanywa na shirika la cement la Iraq kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, imetokana na sauti za kutaka kuwasaidia na kusimama pamoja na familia za mashahidi kwa ajili ya kuonyesha thamani ya kujitolea kwao katika kuhifadhi nchi na maeneo matukufu ya nchi yetu kipenzi pia kama sehemu ya radi amali ya dini kutokana na ushujaa wa majemedali wao.

Baada ya kusomwa Qur’an ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, uliimbwa wimbo wa taifa halafu ukafatiwa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha ikafata khutuba ya Atabatu Abbaiyya iliyo somwa na Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawiy kutoka katika kitengo cha dini, miongoni mwa aliyo sema ni: “Mwanadamu anapo fanya kitu chenye thamani hujifaharisha nacho mbele za watu, hususan kitakapo kua ni cha thamani zaidi kama vile kujitolea nafsi, sisi leo hii tunasimama kwa heshima kubwa mbele ya kina baba na kina mama na wajane walio poteza wapenzi wao, hawa mashahidi watukufu ambao damu zao takasifu zimemwagika katika aridhi hii tukufu lau wangerejea tena katika dunia wangesema tuacheni tukapigane tena hadi tufe shahidi kutokana na neema walizo ziona kwa Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika chochote kitakacho tolewa kwa familia za mashahidi, sawa kimetolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu au taasisi zingine ni kidogo sana kwao, wao walijitolea nyama iliyofichwa na maini yao kwa ijili ya kulinda aridhi ya Iraq na watu wake pamoja na maeneo matukufu”.

Halafu ukawasilishwa ujumbe wa shirika la cement la Iraqi ulio zungumzwa na msaidizi wa mkuu wa shirika Ustadh Muhammad Hassan Naaji, ambaye alisema kua: “Ni fahari kwetu kuwatumikia enyi familia za mashahidi, kwa sababu watoto wenu wamejitolea roho zao kwa ajili ya kuipa utukufu nchi yao na raia wake pamoja na maeneo matakatifu, lau kama si wao Iraq isingepata neema ya utulivu na amani, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwafikishe daima kuwatumikia nyie, hii ni heshima kubwa kwa shirika la cement la Iraq kupata nafasi ya kuwatumikia nyie familia za mashahidi, kila tutakacho kupeni hakilingani hata na tone moja la damu ya watoto wenu iliyo dongoka”.

Kisha ikawekwa filamu inayo onyesha namna wairaq walivyo itikia fatwa ya Marjaa dini mkuu ya kuwataka walinde aridhi yao na maeneo matukufu.

Pia rais wa kamati ya mashahidi katika shirika la cement Sayyid Ghaalib Swafi aliongelea ushujaa na ujasiri wa mashahidi watukufu amboa leo hii tuna neemeka kwa sababu yao, na akasisitiza familia za mashahidi zishikamane na subira kwa kupoteza wapenzi wa nyoyo zao kwa ajili ya kuhifadhi Iraq na maeneo matukufu, na akaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusimamia hafla hii, hafla ilimalizika kwa kugawa zawadi kwa familia za mashahidi watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: