Kwa namba mwaka (2016m): Misaada ya kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya kwa wapiganaji wa jeshi na wakujitolea pamoja na mashahidi na majeruhi wao..

Maoni katika picha
Kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kiwango ilicho toa katika mwaka uliopita wa (2016m) katika kuwasaidia wapiganaji wa serikali na wale wa kujitolea pamoja na familia za mashahidi na majeruhi kimefikia dinari (1,323,568,000) bilioni moja na milioni mia tatu ishirini na tatu laki tano na sititi na nane elfu dinari za kiiraq, pesa hiyo ilitokana na masanduku ya msaada ya Alkafeel yanayo simamiwa na kamati maalum ndani ya kitengo cha dini, kamati hiyo husimamia uwekaji na ufunguaji wa masanduku ya saidia mujahidina na familia zao pamoja na kuhesabu pesa iliyo patikana, hii ni moja ya shughuli muhimu zilizo fanywa na kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu mwaka (2016m), jambo hili ni dogo kimtazamo lakini linafaida kubwa, pia ni miongoni mwa ratiba za kamati ya dini ya Atabatu Abbasiyya iliyo jiwekea kuanzia siku ya kwanza ya kutangazwa kwa fatwa tukufu ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, ambapo ratiba ilikua kama ifuatavyo:

  • 1- Kulisaidia jeshi na hashdi sha’abi kwa hali na mali katika uwanja wa vita na katika maeneo yaliyo kombolewa kutoka kwa magaidi wa kidaesh ambapo jumla ilifika (213.068000) dinari za kiiraq, ambapo ilihusisha kugawa miwani ya usiku kwa wapiganaji na mavazi ya kijeshi, vyakula mbali mbali vibichi na vilivyo pikwa, maji, pamoja na vocha za simu, sigara na mafuta uzuri.
  • 2- Kuwasiliana na familia za mashahidi walio uawa kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu wakiwa wameitikia wito wa Marjaa wao mkuu wa dini na kuwapatia misaada, familia zilizo nufaika na ratiba hii zilifika (1,092) na kilitumika kiasi cha (1,083,000,000) dinari za kiiraq, familia za mashahidi hupokea zawadi moja kwa moja wanapo tembelewa katika miji yao au huombwa wafike katika eneo la karibu na makazi yao au ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wakati mwingine hutegemea matashi ya wana familia pindi inapo tokea dharura ya kushindwa kuwatembelea.
  • 3- Kuwasiliana na majeruhi wa jeshi la serikali au hashdi sha’abi, wakiwa katika nyumba zao au hospitalini na kuwapa msaada wa pesa ili ziwasaidie katika mtihani mgumu walio nao, ratiba hii iligharimu (27,500,000) dinari za kiiraq na ilihusisha kuwapa takrima familia za mashahidi kiasi cha (1,000,000) milioni moja dinari za kiiraq kwa kila familia katika mikoa yote ya Iraq, kila jambo lilitekelezwa na idara husika, pamoja na tuliyo sema pia tulitoa zawadi za kipesa kwa baadhi ya vikosi vya wapiganaji wa hashdi sha’abi ambao hawakupokea mishahara kutoka serikalini au kutokana na mazingira ya kibinadamu.

Kumbuka lengo la ratiba hii ni kusaidia wapiganaji wa kujitolea walio itikia fatwa ya Marjaa dini mkuu ya kulinda Iraq na maeneo yake matukufu, na kufanyia kazi maelekeza ya Marjaa dini mkuu yanayo himiza kuwasaidia wapiganaji wa serikali na wale wa kujitolea (hashdi sha’abi) wanao timua vumbi katika kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu na ubinadamu, jambo ambalo linahitaji juhudi ya ziada katika kuendeleza vita hii dhidi ya maadui hawa, hususan hashdi sha’abi wenye upungufu mkubwa wa zana na pesa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: