Wanafunzi wa vyuo na vituo vya kielimu watoa taazia kwa imamu Husseini na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuomboleza kufariki kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s)..

Maoni katika picha
Kama kawaida yao kila mwaka hutoa taazia kwa imamu Husseini na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya shahada ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mwaka huu wameshiriki zaidi ya wanafunzi (3000) kutoka katika vyuo tofauti na vituo vya kielimu hapa Iraq kupitia mradi wa utamaduni wa kijana wa kiiraq wameunda maukibu (kundi) moja la maombolezo, kwa kushirikiana na idara ya mahusiano ya vyuo chini ya harakati za mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo unao endeshwa na Atabau Abbasiyya tukufu.

Matembezi yalianzia katika barabara ya Kibala ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yakenda hadi ndani ya uwanja wa haram tukufu (ya Abulfadhil Abbasi a.s) kisha wakatoka na kuelekea katika eneo la katikati ya haram mbili, waombolezaji walisomo mashairi mengi sana ya huzuni na maombolezo, yaliyo onyesha ukubwa wa msiba, wakatembea hadi katika haram ya imam Hussein (a.s) wakamaliza kwa kufanya majlisi ya taazia ndani ya haram ya imam Hussein (a.s) huki wakinyanyua pendera za Iraq ikawemo moja kubwa kama ishara ya kushikamana kwao na nchi yao na kushikamana kwao.

Ustadh Maahir Khaalid kutoka katika kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu (idara ya uhusiano wa vyuo) alisema kua: “Mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo miongoni mwa shuguli zake ndani ya mwaka hujumuisha harakati za kitamaduni na kielimu, miongoni mwake hufanywa katika vyuo na vituo vya elimu na zingine hufanywa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na miongoni mwake ni vikao vya taazia ambavyo hujikumbusha misiba ya maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kubainisha yaliyo jiri kwao miongoni mwa dhulma na matatizo kwa kushiriki kundi dogo la wanafunzi, ambao huja kila mwaka na hufanya matembezi ya taazia kwa ajili ya kuhuisha ufuasi wao kwa Ahlulbait (a.s) mbele ya kaburi la imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kama sehemu ya kumuenzi bibi Fatuma Zaharaa (a.s) aliye pinga dhulma, hakika yeye ni sawa na taa linalo angazia uhai wao.

Ahmadi Abdulatifu mwanafunzi wa chuo kikuu cha Badgadi alisema kua: “Hakika jambo hili ni zuri sana ni moja ya kiunganishi kati ya wanafunzi na maimamu wao (a.s) tena jambo hili limekuja sambamba na ushindi wa jeshi letu na hashdi sha’abi, hivyo hii ni fursa pia ya kutoa ushirikiano kwa jeshi na hashdi sha’abi wanao endelea na vita vya kuzikomboa aridhi za Iraq”.

Mwanafunzi mwingine kutoka katika chuo cha Basra ndugu Sataar Ahmadi alisema kua: “Hakika kushiriki kwetu katika harakati hizi za taazia kunatupa nafasi mkubwa ya kukumbuka misimamo ya Ahlulbait (a.s) na kukumbuka dhulma aliyo fanyiwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kupata mazingatio katika maswala hayo, hakika dhulma zote zilizo fanyika hapa Iraq ni muendelezo wa dhulma walizo fanyiwa Ahlulbait (a.s) hasa dhulma aliyo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya kama kawaida yake katika kila mwaka, ilijipanga kupokea makundi (mawaakibu) ya azaa ya Faatyimiyya ndani na nje ya mkoa wa Karbalaa, makundi ya kutoa taazia katika msiba huu mkubwa humiminika kwa imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Ataba tukufu imeweka utaratibu maalumu katika swala hili na kuandaa mimbari za kutolea mihadhara ya kidini inayo elezea utukufu na heshima ya bibi Zaharaa (a.s) pamoja na matatizo aliyo pata baada ya kufariki kwa baba yake (s.a.w.w) katika huu mnasaba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: