Maahadi ya Alkafeel ya taaluma na uendelezaji wa vipaji yafanya makubaliano na chuo kikuu cha Twafu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wake..

Maoni katika picha
Maahadi yaa Alkafeel ya taaluma na uendelezaji wa vipaji iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu yanfanya makubaliano ya kushirikiana na chuo kikuu cha Twafu katika mkoa wa Karbala kuendeleza vipaji vya wanafunzi katika sekta ya tanakilishi (Computer) na kuchangia katika kuongeza kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Mkuu wa mazungumzo hayo upande wa Maahadi Alkafeel Ustadh Saamir Falaah Hassan Swafi alisema kua: “Miongoni mwa sera zetu ni kufungua ushirikiano na taasisi za kielimu na kisekula, na haya makubaliano yanadhihirisha jambo hilo, tunafanya haya kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kuchangia katika kuendeleza vipaji vya watu”.

Makubaliano yamehusisha mambo mengi, ikiwa pamoja na kuendeleza vipaji, katika hili tutaandaa masomo na kuyaweka katika selebasi ya kudumu, kwa ajili ya kufundishia wanafunzi walio hitimu na kuongeza vipawa vyao vya kielimu hasa katika fani mpya, na kutengeneza cd maalumu kwa ajili ya lengo hili, pamoja na kufungua milango ya Maahadi kwa wanafuni na kuwajulisha mambo mapya yanayo ingizwa katika soko la kitaifa na kimataifa, hali kadhalika tutakua na program za kufundisha kiengereza na kifarsi kwa kutumia walimu walio bobea katika sekta hiyo, na tutatoa vyeti vinavyo kubalika kimataifa, pia kutakua na mitihani ya kimataifa kwa wanafunzi wa chuo itakayo pelekea wapewe vyeti vya kimataifa vinavyo kubalika na mashirika ya kimataifa, shahada zitakazo tolewa ni pamoja na:

  • - Microsoft certificates
  • - Adobe certificates
  • - Autodesk certificates
  • - IC3 certificates

Pamoja na kutolewa kwa mitihani mingi ya kimataifa inayo kubalika na mashirika ya kimataifa”.

Kuhusu upatikanaji wa program za ufundi muheshimiwa Swafi alisema kua: “Maahadi inaweza kukipatia chuo program zote za kisasa zinazo tumika katika mambo ya kiofisi na kuendesha semina za kuziendesha”.

Dokta Hamza Abdulwaahid ambaye ni mkuu wa chuo alisema kua: “Hakika makubaliano haya ni nyota njema kwa mustakbali wa wanafunzi wa chuo hiki na mji wa Karbala tukufu na Iraq kwa ujumla, hakika sisi tunakaribisha kila jambo zuri la kielimu katika chuo chetu, kupitia makubaliano haya pamoja na aliyo sema ustadh Saamir tunaweza kuzunguka maeneo mbali mbali na kufanya nadwa za kielimu na kujadili kila jambo jipya na la kisasa linalo ingia katika program za tanakilishi (Computer) na kwa kutumia lugha tunayo ona inafaa katika kuongeza kiwango cha elimu cha mwanafunzi, pamoja na kufanya nadwa za utambulisho kwa wanafunzi wa namna ya kufanya mitihani ya kimataifa na namna ya kupata vyeti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: