Kamati ya maandalizi ya kongamano la wanawake la saba sambamba na kongamano la Rabii shahada yatangaza mada za mashindano ya kitafiti..

Miongoni mwa vikao vya kongamano lililo pita
Kamati ya maandalizi ya kongamano la wanawake la saba litakalo fanyika sambamba na kongamano la Rabii shahada la kimataifa na kitamaduni la kumi na tatu imetangaza kufanyika kwa mashindano ya kitafiti ya wanawake, na kutoa wito kwa watafiti na waandishi wa kike kujitokeza kwa wingi.

Mashindano hayo yanalenga mambo yafuatayo:

 • 1- Kuinua kiwango cha elimu kwa wanawake.
 • 2- Kumuunganisha mwanamke na imamu Hussein (a.s) pamoja na fatwa tukufu ya kujilinda.
 • 3- Kuchukua mazingatio kutoka kwa wanawake wa nyumba ya mtume (a.s) na kufata nyayo za bibi Zainabu (a.s) kutokana na msimamo wake katika vita vya Twafu.
 • 4- Kunufaika na imani ya dini aliyo nayo mwanamke kwa kuzingatia kua ndio msingi wa jamii.
 • 5- Kuzipatia maktaba za kiislamu tafiti stahili zinazo elezea tukio la Twafu na kuziingiza katika mikono ya watafiti na wasomaji.

Mada zilizo chaguliwa kushindaniwa ni:

 • 1- Nafasi ya uongozi baada ya kuuawa kishahidi kwa imamu Hussein (a.s) bibi Zainabu (a.s) kama mfano.
 • 2- Nafasi ya mwanamke katika mapambano ya imamu Hussein.. Umu Abdallah (a.s) kama mfano.
 • 3- Kujitolea na kulinda dini pamoja na kuwaangalia watoto na wanawake.. Abulfadhil Abbasi (a.s) kama mfano.
 • 4- Haki za wanawake katika dalili za kisheria na fatwa tukufu ya kujilinda.. bibi Sukaina (a.s) kama mfano.
 • 5- Matangazo ya bibi Zainabu (a.s) na athari yake katika kuleta ushindi wa tukio la Twafu.
 • 6- Uhusiano wa familia za sasa ukilinganisha na familia bora katika uislamu.
 • 7- Kulinganisha kati ya fikra hasi walizo kua nazo maadui na fikra za Kassim bun Hassan (a.s).
 • 8- Msimamo imara wa familia za hashdi sha’abi ukiulinganisha na Ummu Wahabi.
 • 9- Msimamo imara walio nao wakina mama wa mashahidi wa hashdi sha’abi ukilinganisha na kina mama wengine.
 • 10- Khutuba ya wasila iliyo tolewa na imamu Ali (a.s) kuhusu misingi ya malezi.
 • 11- Zana za usafi kwa mtu na jamii.. bibi Zainabu (a.s) kama mfano.

Masharti ya kushiriki katika mashindano haya ni:

 • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kusambazwa na mtu au taasisi nyingine.
 • 2- Uandike kwa kufuata vigezo vya kielimu.
 • 3- Isiwe chini ya kurasa 15 wala zisizidi 30, ziandikwe kwa hati ya (simplified Arabic) na herufi ziwe na ukubwa wa saizi 14, katika karatasi za A4 na utafiti uwekwe katika (CD).
 • 4- Maneno yasiwe zaidi ya 300, na aandike muhtasari wa utafiti utafiti huo.
 • 5- Utafiti utapelekwa pamoja na viambatanishi vyake vyote ikiwemo CV ya muandishi katika idara ya wanawake kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu. Au utumwe katika barua pepe library@alkafeel.net pia unaweza kupiga simu maalumu ya idara ya wanawake (07721136819) mwisho wa kupokea tafiti ni (10 Rajabu 1438h).

Kamati hailazimiki kurudisha tafiti ambazo hazita kidhi vigezo kwa aliye zituma, zitachambuliwa na kushindanishwa kupitia kamati maalumu ya wataalam walio bobea katika shughuli hiyo, kamati imeandaa zawadi kwa washindi watutu wa mwanzo kama ifuatavyo:

 • - Mshindi wa kwanza: milioni moja na laki tano (1,500,000) dinari za Iraq.
 • - Mshindi wa pili: milioni moja (1,000,000) dinari za Iraq.
 • - Mshindi wa tatu: laki tano (500,000) dinari za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: