Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chadhibiti barabara kuu ya Mosul - Tal-afar na kukata ngome ya mwisho tegemezi kwa adui..

Maoni katika picha
Wapiganaji imara wa kikosi cha Abbasi (a.s) asubuhi ya leo tarehe (22 Jamadil Ula 1438h) sawa na (20/02/2017m) wamefanikiwa kudhibiti barabara kuu inayo unganisha upande wa kulia wa mji wa Mosul na Tal-afar, pia wamedhibiti kitongoji cha Siyaji baada ya vita kali na magaidi ya kidaesh na kukata ngome ya mwisho iliyo kua inategemewa na adui, mafanikio haya yamepatikana siku ya pili toka waingie katika vita chini ya kauli mbiu (Tunakuja ewe Nainawa) inayo kusudia kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul.

Habari zinasema kua; kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kiliendesha vita kali kuelekea kijiji cha Sahaji na wakafanikiwa kudhibiti ngome ya mwisho ya maadui iliyo kua ikiunganisha kati ya Mosul na Tal-afar, walifanikiwa kuangamiza idadi kubwa ya gari zilizo jaa vilipuzi na kumfanya adui apate hasara kubwa ya mali na roho.

Tunapenda kusema kua; kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji jana siku ya Juma Pili kilivamia mji wa Arbidi na kikafanikiwa kukomboa milima ya Muhtariqa karibu na kijiji cha Bakhira kutoka mikononi mwa magaidi ya kidaesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: