Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji leo siku ya Alkhamisi (23/02/2017m) kimetangaza kudhibiti milima ya Atwishana upande wa kulia na kushoto kikamilifu, baada ya vita kali iliyo dumu kwa masaa kadha na kuwapa hasara kubwa madaesh ya mali na nafsi.
Habari zinasema kua; wapiganaji wanahamasa kubwa sana na wanashindana katika kusonga mbele na kukomboa maeneo waliyo pangiwa kimkakati katika upande wa kulia wa mji wa Mosul.
Ushiriki wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika vita hii ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul, kunatokana na uzoefu mkubwa walio pata katika vita mbali mbali walivyo pigana kwa kushirikiana na vikosi vingine vya hashdi sha’abi na vile vya jeshi la muungano pamoja na jeshi la serikali vikiwemo na vikosi vingine vya kujilinda.