Hospitali ya rufaa Alkafeel yaanza awamu ya pili ya mradi wa (matibabu bila malipo) na wanufaika waiomba sekta ya afya iige jambo hili..

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel inaendelea na mradi wake wa kibinadamu (matibabu bila malipo) ulio anza mwisho wa mwaka uliopita, unao lenga kutoa huduma za matibabu bure kwa watu wasiokua na uwezo na wenye matatizo ya afya na wale ambao inakua vigumu kwao kwenda katika vituo vya afya kutokana na umbali au kwa sababu nyingine yeyote, mradi huu unahatua mbili:

Hatua ya kwanza: Kuchunguza na kutafiti miji au vijiji vinavyo faa kupeleka huduma hii, kisha hupelekwa jopo la madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali, na hutoa matibabu ya lazima bure na yale yanayo hitaji upasuaji au matibabu makubwa huandikiwa waende kupata matibabu zaidi hospitali.

Hatua ya pili: Kupokea wagonjwa walio andikiwa kwenda hospitali wakati madaktari walipo enda katika maeneo yao kwa ajili ya kupata huduma zaidi kutokana na matatizo yao, ima kupata vipimo zaidi au ubasuaji au matibabu zaidi kutokana na maradhi ya kila mgonjwa.

Baada ya jopo la madaktari wa mradi wa (matibabu bila malipo) kufanya ziara iliyo husisha mji wa Karbala, Qadisiyya, Naswiriyya, Waasitu na Bagdad, leo hii (24/02/2017m) wameanza kupokea wagonjwa walio wakagua katika ziara zao kwa ajili ya kuwapa huduma zaidi kutokana na maradhi ya kila mgonjwa.

Wanufaika wa mradi huu, baada ya kuona ukweli wa waliyo kua wakiambiwa katika miji yao, wameonyesha furaha kubwa sana na wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa uongozi wa hospitali ya Alkafeel, kwa kuendesha mradi ambao umewaondoshea matatizo makubwa yaliyo kua yakiwakabili kiafya, wakatoa wito kwa serikali na wahudumu wa sekta ya afya waige jambo hili kwa ajili ya kupunguza matatizo ya wagonjwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: