Sayyid Swafi: Hakuna kitu bora zaidi ya Qur’an tukufu, na anaye tumia muda wake kwa ajili ya Qur’an anaweza kuilea nafsi yake katika utukufu na tabia njema..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amesisitiza kua hakuna kitu bora na kitukufu zaidi ya maarifa ya Qur’an, na anaye tumia muda wake kwa ajili ya Qur’an atambue anatumia muda wake kwa ajili ya akhera, anaipendelea nafsi yake pepo na kuiweka mbali na moto, ataweza kuilea nafsi yake katika utukufu na tabia njema.

Aliyasema hayo katika khutuba yake aliyo toa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu yaliyo andaliwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh wa Qur’an tukufu katika Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akasema kua: “Kuna mafanikio yaliyo fikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa mafanikio hayo ni Maahadi ya Qur’an ambayo inajishughulisha na mambo ya kitabu cha Mweyezi Mungu na hii ni safari ndefu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, utakapo fanya kazi na Qur’an tukufu tena kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), hakika kujishughulisha na Qur’an tukufu ni kuufanyia kazi wasia wa mtume Muhammad (s.a.w.w), alipo husia umma wake ushikamane na Qur’an tukufu na akasema kua ni kamba muhimu na kitu cha pili akahusia ushikamane na kizazi chake kitakasifu (a.s), na sisi tunaona kua hizi nguzo (kamba) mili hazitengani, kuna baadhi ya miradi ya tafsiri waliyo anza kuitekeleza ndugu zetu watukufu kisha wakaingia katika maswala ya kizazi kitakasifu, hivyo tunaweza kusema kua ndugu zetu wanaofanya kazi katika Maahadi ya Qur’an ni watumishi wa Qur’an na kizazi kitakasifu ukiongeza na kunasibishwa kwao na hii sehemu tukufu ambayo ni utumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Ndugu zetu wanao fanya kazi katika Maahadi sawa wale walioajiriwa au wanao saidiana nao wana heshima kubwa sana, na yatupasa tuwashukuru kwa kila kazi wanayo fanya, wanafanya kazi mwaka mzima hasa kipindi cha likizo za wakati wa baridi wao huongeza vitindi vya kazi zaidi kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi Qur’an katika viwango vyote, na wala hawashughuliki na wanaume peke yao, wana vitengo vya wanawake pia katika maeneo mbalimbali ambavyo vinajukumu la kukuza uwezo wa masomo ya Qur’an kwa wanawake”.

Akasema: “Tunatamani kuona watoto wetu wanapo fumbua macho wanakutana na Qur’an na waishi katika mazingira ya aya za Qur’an ili kuwafanya waipende, bila shaka familia bora ina athari nzuri kwa kuwaelekeza watoto wao katika mwenendo sahihi na kuwafanya washikamane na Qur’an tukufu (kusoma katika udogo ni sawa na kuandika katika jiwe) athari yake hubaki muda wote atakao ishi mwanadamu hapa duniani, hususan yatakapo kua malezi hayo ni ya kifamilia au kishule na yakaendana na kipaji cha mtoto, tatizo la watu wengi utakuta anakipaji fulani lakini mazingira anayo ishi hayaendani na kipaji chake wala hayampi nafasi ya kukuza kipaji hicho, hivyo unakuta kipajia kinapotea kidogo kidogo hadi kinaisha kwa sababu kimekosa malezi, maimamu watakasifu (a.s) wanatuhusia kuzingatia malezi katika hatua zote, hadi mtoto afikie umri wa kujua jambo zuri na linalo faa kwake kimalezi, mama, baba na mwalimu wana nafasi kubwa sana ya kutambua kipaji cha mtoto”.

Mwishoni alisisitiza kua: “Hakuna kitu bora na kitukufu kushinda maarifa ya Qur’an tukufu, anaye tumia muda kwa ajili ya Qur’an sawa na kutumia muda kwa ajili ya kujenga akhera yake, anaipendelea nafsi yake pepo, na anashughulika kwa ajili ya kuingia peponi na kuitenga mbali na moto, anaweza kuilea nafsi yake katika utukufu na tabia njema, hakuna kazi iliyo bora zaidi ya hii, ambaye ataweza kuendana na kizazi kitakasifu hakika Qur’an ipo pamoja na kizazi cha mtume na kizazi cha mtume kipo pamoja na Qur’an”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: