Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya yafanya mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Asubuhi ya siku ya Ijumaa (26 Jamadil Ula 1438h) sawa na (24/02/2017m) imeanza ratiba ya mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu yanayo simamiwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidhi wa Qur’an katika Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushiriki watu (60) kutoka katika matawi ya Maahadi ndani na nje ya Karbala, ratiba hii inatokana na mradi wa kitaifa wa kuandaa mahafidh wa Qur’an tukufu.

Hafla ya ufunguzi ilifanyika katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ilipata mahudhurio makubwa, akihudhuria pia kiongozi mkuu kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu na naibu katibu mkuu pamoja na idadi kubwa ya viongozi wa vitengo vya Ataba wakiwemo wapenzi wa Qur’an tukufu pamoja na washiriki wa mashindano haya.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha maalumu kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu akaongea mkuu wa Maahadi shekh Jawadi Nasrawi ambaye alizungumza kuhusu harakati za Maahadi na kuzigawa sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza: Utafiti kuhusu Qur’an, sehemu hii inasimamiwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, miongoni mwa kazi zake ni:

   • 1- Kuchapisha msahafu mtukufu, na ndio msahafu wa kwanza kuandaliwa na kuchapishwa na wairaq.   • 2- Kuandaa selebasi za kufundishia masomo ya Qur’an kama vile muongozo wa mwalimu na vinginevyo.   • 3- Kuandaa mtiririko wa visomo vya Qur’an.   • 4- Kuandika tafsiri kwa mujibu wa riwaya za Ahlulbait (a.s).   • 5- Msahafu wenye kutamka na tafsiri yake.Sehemu ya pili: Usomaji wa Qur’an, sehemu hii inasimamiwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidhi wa Qur’an tukufu, miongoni mwa matunda yake ni hawa mahafidhi wa Qur’an mnao waona mbele yenu, miongoni mwa majukumu ya kituo hiki ni:

   • 1- Kuendesha semina za Qur’an wakati wa baridi (kipupwe).   • 2- Kuendesha semina za takhasusi za Qur’an.   • 3- Kuendesha mashindano ya Qur’an ya kitaifa na kimataifa.   • 4- Kuendesha semina za kusoma Qur’an yote.   • 5- Kulea vipaji vya wasomi wa Qur’an na kuviendeleza.   • 6- Mradi wa kitaifa wa kiongozi wa wasomi.   • 7- Kuendesha semina za Qur’an kwa watumishi wa Ataba tukufu.   • 8- Mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomi wa Qur’an, ambao umegawanyika sehemu mbili: usomaji wa kuangalia na kuhifadhi”.Akaendelea kusema kua: “Kuhusu hifdhu tumesha fanya semina katika matayi yote ya Maahadi na kuwapatia vifaa vitakavyo wasaidia katika kuhifadhi Qur’an tukufu, kutokana na utaratibu uliowekwa na kituo, wanaanza kuhifadhi juzuu la kwanza hadi wamalize Qur’an yote, tayali wapo ambao wamesha hifadhi juzuu ishirini, wanatakiwa wamalize kuhifadhi Qur’an yote ndani ya miaka mitano, kwa kuhifadhi juzuu tano kila mwaka, na mashindano haya yanatokana na juhudi zilizo fanywa na kituo hiki katika kuhifadhisha Qur’an tukufu”.

Kisha akazungumza kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ambaye alisema kua: “Hakuna kitu bora na kitukufu kushinda Qur’an tukufu, anaye tumia muda kwa ajili ya Qur’an sawa na kutumia muda kwa ajili ya kujenga akhera yake, anaipendelea nafsi yake pepo, na anashughulika kwa ajili ya kuingia peponi na kuitenga mbali na moto, anaweza kuilea nafsi yake katika utukufu na tabia njema...".

Kisha akaongea jaji wa Qur’an Ustadh Qassim Hami, akasherehesha kwa ufupi kuhusu mambo watakayo tazama katika mashindano, ambayo ni: kusoma kwa kuangalia, kusoma kwa ghaibu (kuhifadhi), sauti, naghma (mvumo wa sauti), kusimama na kuanza, kila kitu kina max zake, na maswali yameandaliwa kutokana na vitu hivyo.

Washiriki wakaanza kuulizwa maswali kama ilivyo pangwa na kamati ya mashindano, mashindano haya yanahusisha matawi yote ya Maahadi ya Qur’an tukufu ndani na nje ya Karabala, kutakua na vikao vinne, mashindano yataisha kesho siku ya Juma Mosi na matokeo yatatangazwa katika hafla itakayo fanyika ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: