Kituo cha turathi cha Basra chashiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa (Mustafa Duwaliyyu ya saba)..

Maoni katika picha
Kituo cha turathi cha Basra kilicho chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa (Mustafa Duwaliyyu ya saba) yanayo simamiwa na uongozi mkuu wa mazaru za kishia tukufa za Iraq kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Basra, yanayo fanyika katika ukumbu wa maktaba kuu ya chuo kikuu cha Basra, huu ni miongoni mwa ushiriki mwingi unaofanywa na kituo hiki ndani na nje ya mkoa.

Kituo kimeshiriki kwa kuonyesha vitu tofauti, vitabu na majarida yanayo husu turathi za Basra pamoja na vipeperushi na folda zinazo tambulisha kituo.

Maonyesho yamepata mahudhurio makubwa ya walimu na wanafunzi wa vyuo pamoja na wageni kutoka nje ya chuo, walionyesha kufurahishwa na maonyesho ya kituo cha turathi cha Basra kutokana na utajiri mkubwa wa historia ya mkoa huu kilio nao, watu walisisitiza kua maonyesho haya yanatukumbusha matukio na historia kwa wakati mmoja.

Ufunguzi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa (Mustafa Duwaliyyu ya saba) umefanyika sambamba na kumbukumbu ya kufariki kwa swahaba mtukufu Khalid Zaid bun Suhani (r.a) chini ya usimamiza wa uongozi mkuu wa mazaru za kishia za Iraq kwa kusaidiana na chuo kikuu cha Basra, na kushiriki zaidi ya vituo (54) vya usambazaji kutoka katika nchi za: Iraq, Iran, Lenanon, Misri, Jodan, Sirya, Kuwait, Imarati na Baharain, maonyesho yalipambwa na vitu tofauti, pamoja na majarida ya uhandisi, ukulima, lugha pamoja na vitabu vya dini, pia kulikua na tawi la wanawake na la watoto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: