Jopo la shamba boy wa Alkafeel wazalisha mimea mipya ya msimu na ya majumbani na yatangaza utayali wake wa kuandaa maeneo ya kitaifa ndani na nje ya mkoa..

Maoni katika picha
Jopo la shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wametangaza kuzalisha na kuingiza mimea mipya ya miche ya msimu na ya kudumu inayo endana na mazingira ya hewa ya mkoa wa Karbala na mikoa mingine kwa ujumla, kazi inaendelea ya kuzalisha mimea zaidi ya miti ya majumbani, maua ya kupamba bustani na barabara za miji yetu kuifanya iwe na mandhari nzuri inayo pendeza machoni na kuvutia.

Kiongozi wa shamba boy wa Alkafeel ustadh Muayyad Hatifu Muhammad alibainisha kua: “Hakika katika idara yetu kazi huendelea mwaka mzima, hakuna kipindi ambacho hupumzika, na tunafanya kazi kwa mujibu wa ratiba ya muda iliyo pangwa, kutokana na uchache wa mimea ambayo hupandwa wakati wa baridi, tuliamua kuagiza mimea mipya na kuizalisha kwa wingi mimea mingine kama vile ile ya miti mikubwa na midogo, pia mimea ya msimu pamoja na miti ya kivuli, hadi tumefikisha aina (35) za miti na mimea tofauti, aina (10 – 12) ni zile muhimu, miongoni mwake ni: (Batunia, Qahwaan na Yaldazu) na miti ya Tafishia, Akasia, Fistulia na miti ya Swanbur, Kharnubu, miti ya Khufu ya ngamia, na miti ya Bambuksi malsaau na mingineo”.

Akabainisha kua: “Wakati uliopita tulipata muitikio mkubwa, kwa sababu nyingi, miongoni mwake ni: Ubora wa mimea, uzuri wa kuamiliana, kujali muda, na kwakua tuna wakala maalumu wa mbegu, Atabatu Abbasiyya tukufu ndio sehemu pekee inayo zalisha baadhi ya miti kwa kiwango kikubwa, na imetenga muda kwa ajili ya kilimo cha miti”.

Akaendelea kubainisha kua: “Kuna mimea ya kudumu inaishi hadi miaka (60) mfano (Jahannami Mutwa’ami) nao ni mmea unaozalishwa katika Atabatu Abbasiyya pekee hapa Iraq, na uliagizwa kutoka nchini Tailand, upekee wa mmea huu huweka maua ya aina tofauti tofauti”.

Mwisho wa maneno yake Ustadh Muayyad, alitangaza utayali wao wa kupamba maua na miti katika maeneo ya kitaifa na mabarabarani hapa Karbala na katika mikoa mingine, kwa kuweka maua na miti inayo endana na mazingira halisi ya hewa, pia kutokana na mapendekezo ya wakazi wa maeneo hayo kupitia katika vituo vya mauzo ya moja kwa moja, kazi hiyo wanaweza kuifanya kwa bei nafuu tofauti na wale ambao huagiza kutoka nje.

Kumbuka kua jopo la shamba boy wa Alkafeel wanazalisha miche kwa wingi, ya msimu, ya kudumu, ya kivuli, pamoja na miti ya mapambo na mimea ya kutambaa aridhini, pia wanazalisha mbolea ya samadi chini ya wataalamu walio bobea katika fini za kilimo wakiwemo wahandisi na wasanifu wakubwa, jambo hili ndio linalo sababisha kuzalisha mimea bora.

Kwa kuwasiliana na shamba boy wa Ataba tukufu unaweza kutembelea ofisi zao zilizopo katika mkoa wa Karbala tukufu, barabara ya Husseiniyya karibu na dude (Qantara) nyeupe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: