Waziri wa ulinzi wa Iraq Arfaan Muhammad Alhayaliy amesifu ushujaa wa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wanao pigana bega kwa bega na jeshi la Iraq katika kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul.
Aliyasema hayo alipo tembelea wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) karibu na milima ya Atwishana akiongozana na mkuu wa majeshi pamoja na mkuu wa opresheni hiyo ya (Tunakuja ewe Nainawa) wakiwa pamoja na mkuu wa upelelezi.
Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidiy, ambaye aliupokea ugeni huo alisema kua: “Hakika lengo la ziara hii ni kukagua hali ya vita inayo endelea sasa hivi na kusikia moja kwa moja kutoka kwa wapiganaji wenyewe mafanikio wanayo pata dhidi ya magaidi wa daesh, waziri alisifu juhudi zinazo fanywa na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali pamoja na kikosi cha Abbasi (a.s) na akasema kua yuko tayali kuwasaidi kitu chochote wanacho hitaji.
Naye kiongozi mkuu wa vikosi vya hashdi sha’abi Haji Hadi Al-amiliy alisifu uzoefu mkubwa wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika kushirikiana na jeshi la Iraq wakati wa vita ya kukomboa upande wa kilia wa mji wa Mosul, alipo tembelea wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) na kusema: “Ushirikiano baina ya jeshi la serikali na hashdi sha’abi ni jambo zuri na muhimu sana, linawakatisha tamaa maadui wanaotaka kutenganisha baina ya jeshi na hashdi sha’abi” akasisitiza kua: “Jeshi na hashdi ni nguvu moja inayopigana bega kwa bega, kama wanavyo pigana pamoja na jeshi la umoja katika maeneo mengi, hakika ushirikiano utaendelea pamoja na kikosi cha Abbasi (a.s) hadi kuutenganisha kabisa mji wa Tal-afar na Mosul na tutaenda Tal-afar kwa kutumia upande wa Mashariki”.
Mwishoni mwa ziara hii, kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidiy alisema kua: “Hakika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinawakilisha hashdi sha’abi katika vita ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul, huu ni ujume kua hakuna vita vinayo weza kuendeshwa bila ushiriki wa hashdi sha’abi kutokana na uwezo walio nao ambao unaonekana wazi katika uwanja wa vita.