Zawadi kubwa ya mashindano ya Mahadawiyya ya tano yawasili katika mji wa Zubair mkoani Basra..

Maoni katika picha
Kamati inayo andaa mashindano ya Mahadawiyya ya tano imetangaza kuwasiri katika mkoa wa Basra mji wa Zubair zawadi kubwa itakayo tolewa katika mashindano hayo, ambayo ni gari za aina ya (Sotana 2017)..

Zimewasili katika vituo vya kupokea vocha (copon) za ushiriki vilivyopo katika mji wa Zubair ambavyo ni:

  • 1- Kamati ya wachinjaji/ maduka ya Kuut.. jirani na shue ya upili (sekondari) ya wasichana ya Zubair, unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba: (07807567843) au (07722015663).
  • 2- Vinapo uzwa vyakula vitam tam (halawiyaat) eneo la Shirini Zubair/ barabara ya Jaahizah.

Yamewekwa mabango mbalimbali yanayo tangaza maonyesho haya na lengo la kufanyika kwake.

Kumbuka kua kamati ya maandalizi ilitangaza kuongeza muda wa kupokea vocha (copon) za ushiriki katika mashindano, ambapo tarehe ya mwisho itakua (1 Shabani 1438 h) sawa na (28/04/2017 m) na siku ya kupiga kura na kutangazwa washindi itakua siku ya Juma Tano (20 Shabani 1438 m) sawa na (17/05/2017 m), walisisitiza kua watu wajibu maswali ya mashindano kwa utaratibu na umakini.

Tunapenda kukumbusha kua mapato yatakayo tokana na mashindano haya yatapelekwa katika miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na katika kusambaza tamaduni za Mahadawiyya, namna ya kushiriki; nunua vocha (copon) yenye maswali kuhusu imamu Mahadi (a.f) na utapata namba yako maalumu ya ushiriki, thamani ya vocha (copon) ni dinari elfu kumi za kiiraq, itapigwa kura ya kuwatafuta washindi katika hafla ya kitaifa siku ya mwisho wa mashindano haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: