Kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu: jumba la vitabu vya mfano la kitaifa lafanya maonyesho ya vitu nadra na nakala kale za kihistoria..

Maoni katika picha
Kwa mnasaba wa siku ya turathi za tamaduni za waarabu, jumba la vitabu vya mfano la kitaifa chini ya wizara ya utamaduni ya Iraq kwa kushirikiana na kituo cha kukarabati na kutunza nakala kale cha Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya jana Juma Tatu (8 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (07/03/2017 m) wamefanya maonyesho ya vitu nadra na nakala kale za kihistoria ndani ya ukumbi wa dokta Ali Wardi katika jumba hilo, maonyesho yalihusisha picha za vitu nadra na nakala kale za kihistoria na namna ya kurepea vitabu, pia palikua na vitabu, nyaraka na majarida ambayo yalirepewa na kituo hicho, maonyesho haya yamefanyika sambamba na kuuchagua mju mkuu wa Bagdad kua miongoni mwa miji ya kibunifu.

Maonyesho yalipata muitikio mkubwa na yalifunguliwa kwa mwimbo wa taifa kisha wakaongea wahadhiri mbalimbali, mzungumzaji wa kwanza alikua ni muwakilishi wa zamani wa wizara ya utamaduni Ustadh Jabir Jaabiriy, ambaye alisema kua: “Hakika manufaa yanayo patikana kati ya turathi za Atabatu Abbasiyya tukufu na jumba la vitabu vya mfano la kitaifa yanatokana na uwezo wa turathi hizo, kwa mfano imamu Abbasi (a.s) anaupekee wake, amefundisha vizazi ya kwamba ni bora kufa na kiu kwa ajili ya kulipa maji taifa, Ataba tukufu zimetoa mafunzo bora kwa taifa, tunatarajia mafanikio haya yaendelee na uwezo uongezeke hasa katika nyaja za utunzaji wa vitabu, herufi na matamko”.

Baada ya hapo aliongea kiongozi mkuu wa jumba la vitabu vya mfano la kitaifa dokta Alaau Abuu Hassan alizungumzia uelewa wa wairaq na namna wanavyo weza kuathiri tamaduni za walimwengu: “Sehemu hii huzingatiwa kua chombo cha kutunza na kulinda tamaduni na turathi za wairaq, na huchukuliwa kua sehemu halisi ya historia ya Iraq katika zama zote, tunajitahidi kutunza tamaduni na kuzirithisha kwa vizazi vingine ili kujenga fikra bora na kuzienzi fikra za watu walio buni mambo mazuri, kwa sababu tamaduni zinatokana na ubunifu na hupepea juu ya aridhi ya taifa, hakika tumefanya kila tuwezalo kulinda tamaduni za kiiraq na kiarabu na kuzitunza kama inavyo hitajika”.

Kisha akafuatia mzungumzaji kutoka katika ofisi ya Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Mahmood Swafi, alielezea nakala kale walizo nazo ambazo huwashangaza wataalamu wa nchi za kiarabu na zisizo kua za kiarabu walio tembelea makumbusho ya Alkafeel, alisema kua: “Hakika maonyesho haya ni dalili ya wazi kwa kila mwenye kuitweza (kuidharau) Iraq, hakika Iraq ni taifa kubwa na itaendelea kua muhimu kieneo, dalili ya hayo ni hazina kubwa tuliyo nayo ya nakala kale na picha halisi za zamani zilizopo katika jumba la vitabu hali kadhalika katika maktaba ya Abbasiyya, hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi kubwa ya kushirikiana na kila ambaye yupo tayali kushirikiana nasi, mfano mzuri ni kufanyika kwa maonyesho haya”.

Akaongeza kusema kua: “Tunacho taka kukibainisha kwa walimwengu ni kua; Ataba za Iraq zina maktaba, nakala kale na turathi mbalimbali, pia zina vituo vya utamaduni vinavyo husisha vitu vingi vya tamaduni za kiiraq”.

Mzungumzaji wa mwisho alikua ni muwakilishi wa wizara wa sasa Ustadh Fauzi Atrushi, alisisitiza umuhimu wa kutunza turathi, kwa sababu turathi huwakilisha historia ya umma uliopita wasasa na hutoa picha ya umma ujao, kisha wahudhuriaji wakaelekea katika sehemu ya maonyesho, miongoni mwa wahudhuriaji alikuwepo pia rais wa wakfu shia Sayyid Alaau Mussawiy ambaye aliyasifu maonyesho haya na akasifu nakala kale na machapisho yaliyopo katika maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: