Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu: Kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni ni jambo zuri na linapasa kueneza fikra zake katika mataifa mengine..

Sehemu ya utoaji wa mialiko
Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya Sayyid Nizaar Hablulmatiin (d.t) amesisitiza kua kongamano la Amirulmu-uminina la kitamaduni ambalo hufanywa kila mwaka na Atabatu Abbasiyya katika nchi ya India ni jambo zuri ambalo hukuza hisia ya maelewano kati ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na watumishi wa Ataba tukufu na hujenga milango ya mawasiliano baina yao.

Aliyasema hayo, alipo kabdidhiwa mualiko rasmi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu wa kumuomba ashiriki katika kongamano litakalo fanyika katika Husseiniyya ya utukufu wa wanawake (Fadhilu Nnisaai) katika mji wa Kalkata nchini India kuanzia tarehe (14 – 19) Rajabu (1438 h) chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirulmu-uminina (a.s) ni hoja kwa waja na muongoaji katika wema), kama sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mlango wa elimu ya Mtume (s.a.w.w) imamu Ali (a.s).

Aliongeza kusema kua: “Hakika makongamano haya ya kitamaduni yana athari kubwa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kutambulisha fikra na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa upande mwingine yanasaidia kujenga hali ya mawasiliano ya kiroho baina yao na malalo ya maimamu wao (a.s) hapa Iraq, ukizingatia kua ndoto zao ipo siku watanawirisha macho yao kwa kuyaona na kuyatembelea”.

Akamalizia kwa kusema: “Tunatamani Ataba zipanue wigo wa kufanya makongamano kama haya katika nchi zingine pia, kama vile China, Indonesia… wao pia wanaishi na shauku ya kutaka kuwasiliana na maeneo haya matukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu wasimamiaji wa kongamano hili wafikie malengo ya kufanyika kwake na awawezeshe kuacha athari nzuri inshallah”.

Kumbuka kua kamati ya maandalizi ya kongamano hili ilitangaza kua; maandalizi ya kongamano yalianza muda mrefu, kwa ajili ya kulinda mafanikio mazuri yaliyo patikana katika makongamano yaliyo pita na kuacha athari kubwa katika miji yaliko fanyika, (mara mbili yalifanyika katika mji wa Lankaar mfululizo na yakafanyika mara moja katika mji wa Haidari Abadi kisha yakafanyika tena katika mji wa Lankaar) imepelekea miji mingine ya India kuleta maombi ya kutaka kongamano hili lifanyike katika miji yao miaka ya mbele kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: