Kukumbuka ukamilifu wa swahaba mkamilifu Ummul Banina (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu yaendesha ratiba ya taazia katika kukumbuka kufariki kwake..

Maoni katika picha
Ummul Banina umetukuka mno utukufu wako, umedumu katika subira na imani utajo wako.

Watoto wako vipenzi walimalizwa katika siku ya Tafu, wakajitolea damu zao takasifu.

Na ukasema maneno yako matukufu yaliyo dumu, yataendelea kunukia harufu nzuri hadi siku ya kuyama.

Ninamlinda Hussein kwa roho yangu na watoto wangu, atakapo ishi Hussein ndio burudisho wa macho yangu.

Hakika alikua mtu mwenye hadhi kubwa aliye chaguliwa na Amirul Mu-uminina (a.s) kua mke wake, akawa mke bora kwake na mama mwema wa watoto wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), huyu mwanamke mtukufu bado sauti yake inagonga aridhini na mbinguni ikiita, Hussein! Abbasi! Ee mateka! (Amani ya Mwenyezi Mungu iwe pamoja nanyi), hakika ni bibi mtukufu, mtakatifu, mama watoto (Ummul Banina) (a.s), ambaye Juma Pili ya kesho (13 Jamadil Aakhira 1438 h) tunakumbuka kufariki kwake, na kujikumbusha ukamilifu wake na kumpa taazia mwanaye kipenzi Abulfadhil Abbasi (a.s), ili kutekeleza wajibu wetu na kuelezea misimamo imara aliyo kua nayo katika kuwanangaza Ahlulbait (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya taazia katika kukumbuka msiba huu wa kukumbuka kufariki kwake (a.s), ratiba itahusisha vitu vingi, miongoni mwake ni:

Kwanza: Kutoa mihadhara ya kidini katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi na jioni itakayo tolewa na mashekhe kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasia, itakayo husu maisha ya mama huyu mtukufu.

Pili: Kumkaribisha muimbaji maarufu Baasim Karbalai atakaye fanya majlisi za huzuni kwa muda wa siku tatu baada ya swala ya Isha ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tatu: Kujiandaa kwa ajili ya kupokea makundi (mawakibu) ya maombolezaji kutoka ndani na nje ya Karbala watakao kuja kutoa pole kwa mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s).

Nne: Kuupamba ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mapambo yanayo ashiria huzuni, taa nyekundu na vitambaa vyeusi.

Tano: Kuendesha majlisi za huzuni katika ukumbi wa kukaribishia wageni (utawala) itatolewa mihadhara ya kidini na Qawsida za huzuni kuhusu Ummul Banina (a.s) kwa muda wa siku mbili.

Sita: Kutoka kundi (maukibu) la waombolezaji la watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kuja kumpa pole Abulfadhil Abbasi (a.s) hapo kesho, kuanzia Atabatu Husseiniyya tukufu.

Saba: Kuandaliwa vipindi maalumu vya kumuelezea Ummul Banina (a.s) vitakavyo rushwa katika redio Alkafeel ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Nane: Kufungua mlango wa kujisajili ziara kwa niaba kwa wale wote walio jisajili katika mitandao yoye ya Alkafeel na kuwafanyia ziara kwa niaba katika kaburi lake huko Baqii, ili kujisajili unaweka kuingia kwa kutumia anuani hii: https://alkafeel.net/zyara/.

Kumbuka kua tarehe kumi na tatu ya mwezi wa Jamadil Aakhira mwaka wa (64 h) ndio alifariki bibi mtukufu Ummul Banina (a.s), jina lake kamili ni: Fatuma bint Hizam Alkilabiyya Al-a’miriyya, anaitwa Ummul Banina kwa sababu ana watoto wanne ambao wote walikufa kishahidi katika mapambano ya Twafu (Karbala) kwa ajili ya kumnusuru bwana wa mashahidi imamu Hussein (a.s). Alifia katika mji wa Madina na akazikwa katika makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: