Atabatu Abbasiyya tukufu yahudhuria ufunguzi wa kongamano la kwanza la kimataifa linalo lenga kuunganisha watu na kueneza amani..

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar ameongoza ugeni ulio hudhuria katika ufunguzi wa kongamano la kimataifa la kwanza linalo lenga kuunganisha watu na kueneza amani, lililo andaliwa na kusimamiwa na kituo cha habari cha kimataifa katika Atabatu Husseiniyya tukufu, asubuhi ya Juma Pili (13 Jamadil Aakhira 1438 h,) sawa na 12/03/2017 m, chini ya kauli mbiu isemayo (Mafundisho kutoka katika uhai wa mtume Muhammad (s.a.w.w) yaujaza ulimwengu amani na usalama) lililo fanyika katika ukumbi wa Khatamul Anbiyaau (s.a.w.w) ndani ya haram ya imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya kuunganisha watu wa aina zote na kufuata mwenendo wa mtume katika kueneza amani na usalama na kuhakikisha watu wa tabaka zote wanalienzi swala hilo hasa viongozi wa kijamii katika magundi tofauti ndani na nje ya Iraq.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i) akaongea, katika maongezi yake alisisitiza umuhimu wa kufuata mafundisho ya mitume ambayo yanasema kua watu wote ni wamoja, na akawataka watu wote washikamane katika msingi huu ambao unalenga kuleta amani na usalama, akaongeza kusema kua: “Hakika maimamu watakasifu (a.s) wanasisitiza jambo hili kwa mujibu wa mafhumu ya riwaya isemayo (Haikua dini isipokua kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) pia kuna riwaya nyingine muhimu ambayo tunatakiwa kuifanyia kazi katika maisha yetu ya kila siku isemayo (Haitakamilika imani ya mmoja wenu hadi ampendee ndugu yake kile anacho kipenda katika nafsi yake na achukie kwa ajili ya ndugu yake kile anacho kichukia katika nafsi yake) na zinginezo, kuna hadithi nyingi zinazo zungumzia kuishi pamoja, sio katika ulimwengu wa kiislamu peke yake bali wa wanadamu wote, leo inalengwa kuvunjwa misingi ya kibinadamu kwa namna tofauti”.

Naye patdri Lobu mkuu wa chuo cha Josefu cha kikatoriki alisisitiza umuhimu wa kufanya makongamano kama haya, ya kuunganisha watu wa dini zote kama sehemu ya kuenzi mafundisho ya mitume wetu watukufu na kuepukana na misimamo mikali iliyo sababisha kuzaliwa kwa makundi ya kigaidi na kitakfiri kama kundi la daesh.

Pia wageni mbalimbali walipata nafasi ya kuzungumza na wote walisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani kati ya makundi yote ya kiislamu na wasio kua waislamu, tushikamane katika yale yanayo tuunganisha, tuishi kwa maelewano na kuweka mbele maslahi ya taifa sio maslahi binafsi wala ya kikundi au dhehebu fulani.

Kiongozi wa kitio cha habari cha kimataifa Ustadh Hassan Ali Kaadhim alisema kua: “Kwa mara ya kwanza linafanyika kongamano lililo husisha wanachuoni wakubwa wa kisunni na ndugu zetu wakristo na idadi kubwa ya wanahabari wa India na Uingereza pamoja na wanahabari wa kiiraq, lengo la kongamano hili ni kuwaleta pamoja watu wote na kupambana na imani kali kwa kusambaza ujumbe wa kuishi kwa amani na usalama”.

Akaongeza kusema kua: “Pembezoni ya kongamano hili kutakua na majadiliano ya kuangalia mazingira halisi wanayo ishi wairaq hivi sasa, pamoja na muitikio mkubwa wa fatwa ya kujilinda iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu, pamoja na nasasha na maelekezo yake kwa wapiganaji katika viwanja vya vita, na kusisitiza kwake kuwasaidia wakimbizi kwa kuwapa mahitaji ya kibinadanu ya lazima”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: